Habari za Punde

Washindi Grande Finale NMB MastaBata wakabidhiwa tiketi, zawadi zao

 

Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Juma Kimori akimkabidhi tiketi ya ndege mshindi wa droo kuu ya MastaBata 'Si Kikawaida' Indra Pratap ambaye ameshinda safari ya kutembelea Mbuga ya Serengeti pamoja na mwenza wake ikiwa imelipiwa kila kitu. Wengine ni Manfred Kayala (Kulia) Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi na Donatus Richard (Katikati mwenye tai) Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishuhudia tukio hilo. Shindano la MastaBata 'Si Kikawaida' lililenga kuhamasisha matumizi ya kadi kwenye manunuzi badala ya fedha taslimu. 
 Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Juma Kimori akimkabidhi zawadi mshindi wa droo kuu ya MastaBata 'Si Kikawaida' Ally Abukari Ally ambaye ameshinda zawadi mbalimbali zikiwemo TV kubwa ya kisasa, friji kubwa na vifaa vingine vingi vyenye thamani ya sh milioni 7. Wengine ni maofisa waandamizi wa benki hiyo wakishuhudia tukio hilo. Sindano la MastaBata 'Si Kikawaida' lililenga kuhamasisha matumizi ya kadi kwenye manunuzi badala ya fedha taslimu. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kadi – Philbert Casmir (Mwisho Kushoto), Donatus Richard Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam (Mwisho Kulia) na Manfred Kayala Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi (anayemfuatia Meneja wa Kanda)

NA MWANDISHI WETU

Washindi 12 wa zawadi kuu ‘Grande Finale’ ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Siyo Kikawaida’ wamekabidhiwa zawadi zao mbalimbali, zikiwemo tiketi za ndege tayari kwa safari za utalii wa ndani katika Mbuga za Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar.

Hafla ya kukabidhi zawadi na tiketi hizo imefanyika jijini Dar es Salaam leo, ambako washindi wawili na wenza wao walikabidhiwa tiketi za safari ya utalii katika Hifadhi za Taifa za Serengeti na Ngorongoro, huku wengine 10 wakikabidhiwa zawadi mbadala zenye thamani ya Sh. Mil. 7 kila mmoja.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori, alisema Kampeni ya NMB MastaBata iliyozinduliwa Novemba 24 mwaka jana, imemalizika kwa mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya watumiaji wa kadi na kwamba jumla ya washindi 436 tayari wamekabidhiwa zawadi mbalimbali.

Kimori alibainisha kuwa, miezi mitatu ya kampeni hiyo, ililenga kuhamasisha matumizi ya kadi za MastaerCard QR, MasterPass, Vituo vya Mauzo (PoS) na mifumo mingine ya kidijitali, ambako kulikuwa na mwitikio mkubwa kwa wateja wao.

Aliongeza kuwa, jumla ya washindi 400 walizawadiwa kiasi cha Sh. 100,000 kila mmoja, huku wengine 20 wakijinyakulia zawadi za simu janja aina ya Samsung Note 20 zenye thamani ya Sh. Mil. 2.4 (kila moja), wakati washindi wa Grande Finale wakijinyakulia zawadi za Sh. Mil. 7 kila mmoja. Mpaka kufikia mwisho, benki ya NMB imetumia shilingi milioni 200 kufanikisha promosheni hiyo

Alizitaja zawadi za washindi wa Grande Finale kuwa ni pamoja na friji kuwa la milango miwili, televisheni kubwa ya Samsung (inchi 55) iliyolipiwa king’amuzi cha DSTv kwa miezi mitatu, microwave, water dispenser kompyuta mpakato ‘laptop’ na simu ndogo ya Samsung.

“NMB tunawapongeza washindi wote 436 pamoja na washiriki wengine wa NMB MastaBata, kampeni iliyolenga kuchagiza matumizi ya kadi na kuacha matumizi ya pesa taslimu mkononi, ambao umekuwa utamaduni hatari kwa sasa” alisema Bwana Kimori

“Wito wetu kwa wateja wote wa NMB ni kuendelea na utamaduni chanya wa manunuzi na matumizi kwa njia za kadi. Kwa sasa matumizi ya pesa taslimu mkononi sio tu ni hatari kwa usalama wa fedha zao, bali pia ni gharama kubwa,” alisema Kimori katika hafla hiyo.

Alisisitiza kuwa kumalizika kwa kampeni hiyo ni mwanzo wa kampeni zingine zinazobuniwa na kutolewa na NMB na kwamba ushindi wa mwaka uliopita wa Tuzo ya Benki Salama Zaidi Tanzania, uwe chachu ya wateja kuendelea kuamini katika matumizi na manunuzi yao ya kila siku.

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, aliwapongeza washindi wa MastaBata waliotoka katika Kanda yake na Tanzania nzima kwa ujumla na kwamba huduma za matumizi kwa kadi unaendelea kupitia Pay E na MastaBata.

Aliongeza kuwa NMB haitolala, badala yake itaendelea na ubunifu utakaozaa huduma mbalimbali zinazojali mahitaji ya wateja wao, ikiwemo manunuzi kwa kadi, aliyosema yataendelea kuwa rahisi, salama na nafuu kwa kila mtumiaji.

Akizungumza kwa niaba ya washindi wengine, Ali Aboubakar Ali, ambaye alichagua zawadi mbadala ya vitu badala ya safari ya utalii, alisema ushindi alioupata kumuwezesha kutwaa zawadi hizo, unathibitisha namna droo za kampeni hizo zilivyozingatia bahati za washiriki.

“Naishukuru NMB sio tu kwa huduma bora nazopata kila siku, bali kwa namna walivyoendesha shindano hili kwa haki, kiasi cha kuniwezesha mimi kuwa mmoja wa washindi. Hakukuwa na ubabaishaji na nakiri kwamba ushindi wangu umetokana na bahati na sio vinginevyo,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.