Habari za Punde

Kuwasilishwa kwa bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala Za Mikoa, Serikali Za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Kwa Mwaka 2021-2022

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akichangia Hutuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kwa mwaka wa fedha 2021/2022, iliowasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohammed, akijibu hajo na michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wakati wa kuchangia Hutuba ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake. kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 

Wakuu Wa Vikosi Vya Idara Maalum Vya SMZ wakifuatilia majadiliano yanayohusu makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi Ya Rais, Tawala Za Mikoa, Serikali Za Mitaa Na Idara Maalum Za Smz Kwa Mwaka 2021-2022 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachofanyika Chukwani.

Wakuu Wa Vikosi Vya Idara Maalum za SMZ wakimpongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Smz  Mhe Massoud Ali Mohammed mara baada ya kupitishwa bajeti ya wizara hiyo bila ya mabadiliko.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.