Habari za Punde

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA MARA BAADA YA KUWASILI NAIROBI NCHINI KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya. leo tarehe 04 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wa nyimbo za Mataifa Mawili ya Tanzania na Kenya zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni Mara baada ya Kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya kuwasili Nairobi nchini Kenya 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.

 PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.