Habari za Punde

Mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari kisiwani Pemba

MWANDISHI wa habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Pemba Thureya Gahalib, akiwasilisha kazi za kundi namba mbili, wakati wa mafunzo ya waandishi wa hawabari Pemba, yaliyoandaliwa na Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar- Zanzibarleo, mafunzo yaliyofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAANDISHI wa Habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari vyenye wawakilishi wake Kisiwani Pemba, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya siku tatu ya uwandishi wa habari, yaliyoandaliwa na shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar- zanzibarleo na kufanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MWANDISHI wa habari Mkongwe na mwandamizi Zanzibar, Salim Said Salim, akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba, wakati wa mafunzo ya siku tatu yaliyoandaliwa na shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar- zanzibarleo na kufanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MHARIRI Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar, Zanzibar Leo Yussuf Khamis akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari Kisiwani Pemba, mafunzo hayo yaliyoandaliwa na shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar-zanzibarleo na kufanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.