Habari za Punde

Uhamiaji watakiwa kulinda mapato

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (wapili kushoto) akiongozana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara yake wakati wa ziara ya kutembelea Mpaka wa Namanga unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya ikiwa ni ziara ya kusisitiza umuhimu wa kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini
Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Namanga,Mrakibu wa Uhamiaji, Prolimina Tairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo, juu ya sehemu ya kupimia afya kwa wageni wanaoingia na kutoka nchini wakati wa ziara ya kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akizungumza na Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Namanga,Mrakibu wa Uhamiaji, Prolimina Tairo(kulia),Afisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji,Hosea Kagimbo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Justine Masejo alipotembelea leo Mpaka wa Namanga unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya ikiwa ni ziara ya kusisitiza umuhimu wa kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini
Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Namanga,Mrakibu wa Uhamiaji, Prolimina Tairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo, juu ya udhibiti wa uingiaji na utokaji nchini kwa wageni na wenyeji wakati wa ziara ya kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo(katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo alipotembelea leo Mpaka wa Namanga unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya ikiwa ni ziara ya kusisitiza umuhimu wa kuimarisha doria na misako ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia na kukamatwa nchini.

Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Abubakari Akida, Arusha

Idara ya Uhamiaji imetakiwa kuongeza kasi,kulinda na kuwa na uadilifu katika ukusanyaji wa mapato yanayotokana na shughuli za kiuhamiaji ili kuweza kulisaidia Taifa katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali katika Kituo cha Namanga ikiwa ni kukagua maeneo yanayotumika kwa uingiaji na utokaji wa wageni na wenyeji  lengo ikiwa kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu wanaokamatwa mikoa mbalimbali nchini.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia anawategemea sana, kwanza katika ulinzi wa nchi, ulinzi wa raia na mali zao, ikifika sehemu tukasema Tanzania ina amani basi nyie askari wetu ndio mmefanya kazi hiyo,mnalinda mipaka yetu usiku na mchana, pili anawategemea katika ukusanyaji wa mapato, nawaomba mapato yote yanayotokana na shughuli za kiuhamiaji muyadhibiti ili yatumike katika kujenga Taifa hili,jiepusheni na rushwa,”alisema Naibu Waziri Chilo

Pia aliwataka askari hao kuongeza kasi ya misako na doria kwa usalama wa nchi yetu ili wananchi waweze kushiriki shughuli zao za kimaendeleo kwa amani na salama ikiwa ni adhma ya serikali kuona wananchi wanafanya shughuli zao kwa amani na usalama.

Akisoma taarifa mbele ya Naibu Waziri,Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha Namanga,Mrakibu wa Uhamiaji, Prolimina Tairo amesema  kumekuwepo kushuka kwa mapato kulikosababishwa na janga la Korona ambako idadi ya wageni wanaoingia nchini imeshuka.

“Kuanzia mwezi Januari mpaka Mei Idara ya Uhamiaji katika Kituo cha Namanga tumekusanya jumla ya Dola za Kimarekani 180,780 tofauti mwaka jana kipindi kama hiki tulikua tumekusanya Dola za Kimarekani 450,000 na kushuka huko kunasababishwa na janga la Korona ambalo linaathiri shughuli za uingaiji na utokaji kutokana na vizuizi vilivyowekwa kwa raia wa nchi mbalimbali wanaopitia katika mpaka huu wa Namanga” alisema Tairo

Jumla ya wahamiaji haramu 11 wamekamatwa katika Wilaya ya Longido wakati wa operesheni ya kukamata wahamiaji inayoendelea katika mikoa yote iliyopo mpakani mwa Tanzania nan chi Jirani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.