Habari za Punde

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar yakamata bidhaa zisizokidhi viwango

Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa vipodozi kutoka Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) Salim Hamad Kasim (wakatikati) akiwa na waandishi wa habari wakitizama tarehe ya mwisho wa matumizi ya tambi aina ya pasta walizozikamata nyumbani kwa mfanya biashara Ramadhani Khatibu Juma Shakani Nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mkaguzi Mkuu wa chakula kutoka Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Sleiman Akida Ramadhan akitoa maelezo kwa wandishi wa habari kuhusu bidhaa walizozikamata nyumbani kwa mfanyabiashara Ramadhani Khatib Shakani.
Wafanyakazi wa Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakifungua mlango wa Godauni la mfanya biashara Ramadhani Khatib liliopo kwa Mombasa kwa Mchina ili kukagua bidaa zilizokuwemo.

 Mkaguzi Mkuu wa chakula Sleiman Akida Ramadhan akiwa na maafisa wenzake pamoja na mfanya biashara Ramadhani wakitizama nyaraka mbalimbali za bidhaa walizozikamata nnje ya Godauni liliyopo kwa Mombasa kwa Mchina.

Picha na Makame Mshenga.


Na Ali Issa Maelezo 18/6/2021


Zaidi ya bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 200 zimekamatwa na Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) kwa kukosa kiwango cha uingizwaji nchini pamoja na kupitiwa na muda.


Akitoa taarifa kwa wandishi wa habari mara baada ya ukaguzi wa  bidhaa hizo Mkaguzi Mkuu kutoka Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Suleiman Akida Ramadhani amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika maeneo ya Shakani na Kwamchina.


Alisema bidhaa hizo zimeingizwa kutokea nchini Ukrain zimeingia Zanzibar bila ya kufanyiwa ukaguzi na Wakala husika jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliowekwa.


Alifahamisha kwamba bidhaa hizo hazikuwa na  vifungashio vyenye lugha inayofahamika na kutoa maelekezo pia zimeshapitwa na muda na ni hatari kwa matumizi ya binadamu.


Akizitaja bidhaa hizo nipamoja na Tambi aina ya Pasta, makoronya, sabuni mbalimbali na biskuti ambazo zimeingia nchini mwaka 2019 na hazikuwahi kukaguliwa kupitia Wakala wa  Chakula, Dawa na Vipodozi.


Mkuu huyo aliwataka wafanyabishara kufuata sheria na taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini ili kuepuka hasara pamoja na kulinda afya ya  mtumiaji.  


“Mfanya biashara yoyote ni lazima akubali maagizo anayopewa na taasisi husika kabla ya kuingiza bidhaa nchini na sio kumuachia wakala kutoa mizigo kinyemela kwani hupelekea hasara pale zitakapoangamizwa” alisema Mkaguzi huyo


Nae Mfanyabiashra wa bidhaa hizo Ramadhani Khatibu Juma amesema amekubali kupokea uamuzi utakaotolewa na taasisi  hiyo ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kumpata mtumiaji.

Aidha alisema kuwa suala la kutokaguliwa bidhaa hizo linatokana na  kumuachia wakala wake ambaye alimthibitishia kuwa amelipia sehemu zote zinazo stahiki kulipiwa na kufanyiwa vipimo kwa matumizi ya binaadamu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.