Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewashu Wananchi wa Jimbo la Konde katika Wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kuendelea kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa jimbo la hilo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema kutokana na imani hiyo ya Wananchi, katika Uchaguzi huo mgombea wa CCM Sheha Mpemba Faki ameweza kushinda kwa kura 1796 ambazo ni za kishindo.
Jimbo hilo lilikuwa chini ya upinzani kwa miaka 15 na kwamba Konde ni Jimbo la tatu CCM kushinda tangu Rais Samia Suluhu Hassan achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.
Shaka amesema, mbali ya kushinda Ubunge jimbo la Konde, CCM imepata ushindi katika Kata 6 katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani Tanzania Bara na kuzitaja Kata hizo kuwa ni Mbagala Kuu iliyopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam na Kata ya Ndirigishi iliyopo Kiteto mkoa wa Manyara.
Kata zingine ni Mitesa iliyopo Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara, Gare iliyopo Wilaya ya Lushoto mkoa wa Tanga, Mchemo iliyopo Wilaya ya Newala mkoa wa Mtwara na Kata ya Chona iliyopo Wilaya ya Ushetu mkoa wa Shinyanga.
"Ushindi huu umetokana na uaminifu na uadilifu wa Chama Cha Mapinduzi katika kuwasikiliza na kuwatumikia wananchi, aidha unatuongezea ujasiri na nguvu zaidi katika kuendelea kuwatumikia watanzania.
CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia kwa usikivu, bidii kubwa amani na utulivu kwa kuwa tunao uzoefu mkubwa wa kufanya hivyo", amesema Shaka na kuongeza;
"Chaguzi hizi zinaendelea kutoa funzo kwa vyama vya Upinzani nchini kuwa wasiendelee kutafuta mchawi bali wakae chini wajitafakari na wajadili mtazamo wa namna wanavyofanya na kuendesha siasa zao, sivyo kama wataendelea kutegemea siasa za ukosoaji wa makosa ya serikali inayongozwa na CCM kwa kutumia hoja ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha basi utawaoandosha katika ramani za siasa nchini".
No comments:
Post a Comment