Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kulia) akishiriki katika Sala ya Maiti ya Marehemu Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dk.Aboud Suleiman Jumbe katika Masjid Mushawal Mwembe shauri Jijini Zanzibar baada ya Sala ya Ijumaa na maziko kufanyika leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) pamoja na waumini mbali mbali na wananchi wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (wa tatu kulia) baada ya Sala ya Maiti ya Marehemu Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dk.Aboud Suleiman Jumbe katika Masjid Mushawal Mwembeshauri Jijini Zanzibar baada ya Sala ya Ijumaa na maziko kufanyika leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini MagharibiRAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, leo amejumuika na
mamia ya waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya sala ya Ijumaa, iliofanyika
Masjid Mushawar, Mwembeshauri Jijini Zanzibar.
Akisoma khutuba ya sala hiyo, Sheikh Mziwanda Ngwali Ahmad amewataka binaadamu kutokusahau neema kubwa waliyozuruzukiwa na Mwenyezi Mungu na kubainisha udhaifu walionao mbele ya Muumba.
Amesema binadamu wanapaswa kutambuwa udhaifu wao unaotokana na maumbile waliyonayo.
Sheikh Mziwanda aliwataka waislamu kumuogopa Mwenyezi Mungu na kudumu katika kufanya mambo mema kwa kutambua utukufu alionao mola wao.
Alisema pamoja na udhaifu walionao binadamu, Mwenyezi Mungu amewatukuza binaadamu na hivyo akatumia fursa hiyo kumuomba Mwenyezi Mungu kuwapa malipo mema waja wake.
Aidha, aliwataka waislamu kuondokana na jeuri na kiburi kwa ajili ya asili zao, nasaba, mali au elimu waliyonayo.
Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi alishiriki katika sala ya kumuombea dua maiti ya mke wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Aboud Suleiman Jumbe, ambae amezikwa mchana huo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Unguja.
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024
2231822
E-mail: abdya062@gmail.com.
No comments:
Post a Comment