RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.
Hussein Ali Mwinyikesho Jumamosi (Julai 03,2021) anatarajia kuanza ziara ya
kikazi ya wiki moja katika mikoa mitatu ya Unguja.
Rais Dk. Mwinyi ataanza ziara yake hiyo katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo ataanza katika Wilaya ya Kusini na kumalizia katika Wilaya ya Kati, baada ya hapo Rais Dk. Mwinyi ataendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na atamalizia katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katika ziara hiyo Rais Dk. Mwinyi anatarajiwa kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji, elimu, afya, umeme, miundombinu ya barabara, bandari, kilimo, uvuvi,maeneo yanayochimbwa mchanga na miradi mengineyo.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi anatarajia kukutana na Wajasiriamali mbali mbali katika ziara yake hiyo ambapo pia atapata fursa ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi katika Mikoa hiyo na hatimae kufanya majumisho kwa kila Mkoa ambao atafanya ziara yake hiyo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment