Habari za Punde

Dk.Hussein Awapongeza Madaktari wa China Wanaotoa Huduma za Afya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraz la Mapinduzi Mhe.Dk. Mwinyi alitembelea hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani na kuwapongeza Madaktari wa kichina wanaomaliza muda wao kwa vile wanatowa huduma katika hiyo na kusema mchango wao ni mkubwa unathaminiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani kuna baadhi ya huduma bila ya mchango wao zengeyumba.

Aidha Dk, Mwinyi aliwapongeza wafadhili waliotowa misaada ya vifaa mbali mbali kwa ajili ya Hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani akiwemo Said Bopar na kusema kuwa misaada hiyo  ni muhimu sana.

Aidha,  alimpongeza na kumshukuru Mwakilishi wa Jimbo la Mkoani Mhe.Abdalla Hussein Kombo kwa kukabidhi gari la kubebea wagonjwa katika Hospitali hiyo ya Abdalla Mzee Mkoani na kuisaidia Serikali yake kwani kwa Hospitali kama hiyo ni muhimu kuwa na gari ya aina hiyo.

Dk, Mwinyi aliwashukuru wafanyakazi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na kusema amesikia matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo kutoka kwa mganga  mkuu wa Hospitali hiyo Dk, Haji Mwita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.