Habari za Punde

Wafanyakazi Uwanja wa Ndege ChakeChake Pemba Wapatiwa Chanjo ya UVIKO 19.

MKURUGENZI wa Rasilimali watu kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Ndg.Rajab Uweji Yakub, akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo Pemba juu ya umuhimu wa Chanjo ya Uviko 19, hafla iliyofanyika katika kiwanja cha Ndege Chakechake Pemba
AFISA Chanjo Wilaya ya Chake Chake Pemba Ndg.Fihim Abdalla Mohamed, akielezea umuhimu wa chanjo kwa jamii wakati alipokua akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Pemba.
Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Pemba (ZAA) Ndg.Rajab Ali Mussa, akichomwa chanjo ya UVIKO 19 na daktari kutoka Hospitali ya Chake Chake Pemba Bi.Asha, zoezi hilo lililofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Chakechake Pemba.
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Pemba Bi.Fatma Said, akichoma chanjo ya UVIKO 19 na daktari kutoka Hospitali ya Chake Chake Pemba kitengo cha Chanjo, hafla hiyo  iliyofanyika katika ofisi za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Pemba.

Mfanyakazi wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Chakechake Pemba Bi.Samira Ali akipata Chanjo ya Uviko -19, kutoka kwa Daktari wa Kitengo cha Chanjo Hospitali ya Chakechake Pemba, zoezi hilo la chanjo lililofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Ndege Chakechake Pemba.

PICHA NA ABDI kutoka kwa SULEIMAN, PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.