Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi atembelea maeneo ya Uwekezaji Micheweni Pemba

MWANANCHI wa Maziwang’ombe Bw. Mbwana Haji akizungumza na kutoa kero yake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika eneo la Uwekezaji Micheweni Pemba.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar.Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga, akitowa maelezo ya Eneo la Uwekezaji Micheweni Pemba wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, ilioanza leo 31-8-2021.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha  Maziwang’ombe Wilaya ya Micheweni akitembelea eneo la Uwekezaji na kuona utekelezaji wa wa agizo lake ya ujenzi wa barabara katika eneo hilo, akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.