Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Ashirikiana na Wananchi Kusafisha Eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya Narungombe Wilayani Ruangwa.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa akishirikiana na wananchi kusafisha eneo la ujenzi wa Kituo cha Afya cha  Narungombe wilayani Ruangwa, Septemba  4, 2021. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Frank Chonya. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa akishirikiana na wananchi kusafisha eneo la ujenzi wa Kituo cha Afya cha Narungombe wilayani Ruangwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa akishirikiana na wananchi kusafisha eneo la ujenzi wa Kituo cha Afya cha Narungombe wilayani Ruangwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa akishirikiana na wananchi kusafisha eneo la ujenzi wa Kituo cha Afya cha Narungombe wilayani Ruangwa, Septemba  4, 2021.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 4, 2021 ameshirikiana na wananchi kusafisha eneo ambalo litajengwa kituo cha Afya Katika kata ya Narungombe, Ruangwa Mkoani Lindi.

 

Akizungumza na wananchi katika eneo hilo Waziri Mkuu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitahudumia wakazi wa Vijiji vya Nangurugai, Machang’nja, Chikwale, Chiundu, Liuguru, Itumbi, Nkoma na sehemu ya Chunyu

 

“Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameamua kuimarisha sekta ya afya kwa kuimarisha vituo vyote vya kutolea huduma, kituo hiki litawekwa eneo la kupokea wagonjwa na sehemu ya madaktari hadi watano kusikiliza wagonjwa”.

 

Amesema kuwa “Kutakuwa na maabara kubwa, jengo la mama na mtoto ikiwemo chumba cha upasuaji, kutakuwa na eneo la watoto njiti na kutakuwa na jengo kwa ajili ya upasuaji mdogo, wa kati na mkubwa”.

 

Aliongeza kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya kituo hicho, Rais Samia ameahidi kuwa atatoa shilingi milioni 250 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa ikiwemo vya  upasuaji na vipimo.

 

Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Mwenyekiti wa Kijiji Narungombe Rashidi Omari Chijuni kuunda kamati kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa kituo hicho ili kuhakikisha ujenzi wake unakamilika katika muda uliokusudiwa “tuoneshe umakini katika hili, wananchi hawa wote wanahitaji huduma kutoka katika kituo hiki”

 

Akiongea kwa niaba ya Wazee wa Kijiji cha Narungombe Mzee Selemani amewashukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Narungombe.

 

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakazi wa kijiji hicho wamemshukuru Rais Samia kwa kuamua kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, kwani kitawapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma za afya.

 

Awali, Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa Ghala ya kuhifadhia mazao la Chama cha Ushirika cha RUNALI na baadae kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA.

JUMAMOSI, SEPTEMBA 4, 2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.