Habari za Punde

TANZANIA COMMERCIAL BENKI PLC WATOA MSAADA WA SARUJI MIFUKO 100

Paroko wa Parokia Padri Ponciano Kibobera wa Kanisa la  Katoliki Ipuli Mkoani Tabora aliyefavaa kazuu nyeupi akipokea saruji mifuko 50 kutoka kwa meneja wa benki Timony Joseph  tawi la Tabora

Na Lucas Raphael,Tabora

Benki ya Tanzania Commercial Benki  PLC (TCB) Mkoani Tabora imetoa msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa shule ya seminari ya Itaga na Kanisa katoliki Ipuli  kwa ajili ya kufanikisha ukarabati  majengo ya shule na kumalizia kanisa hilo iliyoghalimu kiasi cha shilingi milioni 2


Akitoa msaada huo Meneja wa Tawi la Benki hiyo mkoani hapa Timony Joseph alisema benki ilifikia uhamuzi wakutoa msaada wa mifuko 100 ya saruji katika shule na kanisa  ikiwa ni moja ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani katika suala zima la elimu na kuabudi.


Meneja huyo alisema  pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali lakini shule hiyo ni wadau wakubwa wa kuweka fedha zao katika benki ya TCB hivyo saruji waliyoitoa itasaidia kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo.

Alisema miundimbinu ya shule inapokuwa mizuri inasaidia kwa wanafunzi kusoma masomo yao vizuri ikiwa pamoja na kuongeza vipaji vya elimu.

Akizungumza mara baada ya kupokea mifuko 50 ya saruji Mkuu wa Seminari ya Itaga, 
Gombera Padre Joseph Buhili alisema anaishuru benki hiyo TCB kwa kuamua kutoa saruji hiyo ambayo ni tendo la kiungwana la kuwajali na kuona umuhimu wa elimu.

Padri huyo alisema kwamba wameupokea msaada huo kwa mikono miwili na utatumika kwa  kukarabati majengo ya shule hiyo kwa ajili ya kuwezesha watoto kusoma sehemu  salama.

Aidha alisema kupatika kwa saruji hiyo kutasaidia na wadau wengine kuamua kujitokeza na kutoa msaada kama huo kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule hiyo ambapo  mwakani inatimiza miaka 100.

Alisema shule ya Itaga seminari inajumla ya wanafunzi 230 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita ambao wanafunzi masomo ya kiroho na kimwili ili baada ya kumaliza masomo yao wakalitumikie Taifa na jamii kwa ujumla.
Naye Paroko wa Parokia ya  Ipuli Padre Ponciano Kibobera aliishukuru benki hiyo  kwa kujali na kuona kanisa nalo linapaswa kupata hisani kwa kutoa mifuko ya saruji 50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.
Alisema kwamba kanisa hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuingia waumini 4000 kwa wakati moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.