Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Isdor Mpango Afungua Mkutano wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Mawaziri  kutoka nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika wakati alipowasili katika Ukumbi wa Hoteli ya Lake Tanganyika Mkoani  Kigoma kwajili ya kufungua  mkutano wa tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza wakati wa ufunguzi mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wanaoshiriki Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika mara baada ya kufungua mkutano huo unaofanyika katika  ukumbi wa mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma. Desemba 16,2021. ( kutoka kushoto kwa Makamu wa Rais ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande, Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira kutoka Zambia Mhe. Collins Nzovu, Waziri wa Mazingira , Kilimo na Mifugo kutoka Burundi Mhe. Deo-Guide RUREMA na Waziri wa Uvuvi na Mifugo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo Mhe. Adrien Bokele).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  wanaoshiriki mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika mara baada ya kufungua mkutano huo unaofanyika katika  ukumbi wa mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma. Desemba 16,2021.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.