Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameongoza Wananchi Katika Kisomo cha Dua na Hitma Kumuombea Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia)

 

Waumini wa Dini ya Kiislam wakisoma kisoma cha hitma kumuombea Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, kisomo hicho kimefanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kabla ya Sala ya kusalia kuusalia mwili wa marehemu.

Waumini wa Dini ya Kiislam wakisoma kisoma cha hitma kumuombea Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, kisomo hicho kimefanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kabla ya Sala ya kusalia kuusalia mwili wa marehemu.

Sheikh Khalid Mohammed Kassim akihitimisha kisoma cha hitma ya kumuombea Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) baada ya kumalizi kisomo cha hitma kilichofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma kumuombea marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, iliofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Uroa Wilaya ya Kati Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameungana na mamia ya wananchi katika maziko ya mwanasiasa   maarufu Marehemu Issa Kassim Issa ‘Baharia’ yaliofanyika kijijini kwao Uroa, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.                                                                          

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariamu Mwinyi alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika maziko hayo.

Wengine waliohudhuria maziko hayo ni pamoja Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar.Mhe Khamis Ramadhan Shaban, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe.Zubeir Ali Maulid,Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Viongozi wa Dini, Wanasiasa pamoja na viongozi mbali mbali na Wananchi wa Zanzibar. 

Aidha, katika maziko hayo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk. Hussein Mwinyi alishiriki katika dua ya kumuombea maiti pamoja na sala iliofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Uroa na badae kufika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa Wanafamilia.

 Akisoma wasfu wa Marehemu Katibu wa Vijana (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja Ndg.Aboud Said Mpate alisema Marehemu Issa Kassim Issa alizaliwa  mwaka 1957 katika Kijiji cha Uroa Wilaya kati Unguja na kupata elimu za msingi na Sekondari hadi Kidato cha Nne (F.IV) katika skuli ya Uroa na hatimae kupata mafunzo ‘Field Engineer Logistic Commmunication’  katika Jeshi la wananchi wa Tanzania.

Alisema wakati wa uhai wake Marehemu alijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977 na kufanikiwa kushika nyadhifa  mbali mbali za Uongozi ndani ya chama hicho, ikiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mbunge wa Jimbo la Mpendae (2005-2010) pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa Kusini Unguja kuazia mwaka 2017, wadhifa aliodumu nao hadi anafikwa na mauti.

Kufuatia kifo hicho Chama cha Mapinduzi Mkoa Kusini Unguja kimetoa mkono wa pole kwa wafiwa, ndugu, jamaa na wanachama wa CCM na Jumuiya zake na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba, sambamba na kumuomba Mwenyezi Mungu kuiweka roho ya Marehemu mahala pema peponi.

Marehemu Issa Kassim Issa aliefariki jana katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ameacha vizuka wawili, watoto 12 na wajukuu saba.

Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.