Habari za Punde

Waziri Jamal Kassim afanya ziara bandarini kuhusu uwepo wa Makontena ya lami yalokuwepo muda mrefu bandarini

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali, wakiwa katika ziara ya pamoja katika Bandari  ya MalindiZanzibar na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali,kuangalia uwepo wa Makontena ya lami yalokuwepo muda mrefu bandarini hapo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali, akielezea kuhusu tatizo lilokuwepo katika eneo la Mizigo Bandari ya Mlindi Zanzibar, kwa kuwepo Makontena ya Lami muda Mrefu wakati alipofanya ziara Bandarini hapo.  
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali, akielezea changamoto zilizopo katika eneo la Mizigo, kwa kuwepo Makontena ya lami kwa muda mrefu katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.

Muonekano wa Makontena ya lami yaliyopo Bandari ya Malindi Zanzibar kwa muda Mrefu.

PICHA NA MARYAM KIDIKO – MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.