Habari za Punde

Waziri Mhe Tabia Maulid Azungumza na Waandishi wa Habari Mafanikio ya Wizara Yake Katika Kipindi cha Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni  na Michezo Mh.Tabia Maulid Mwita akitoa taarifa kwa vyombo vya  habari kuhusu mafanikio ya Wizara yake ndani ya mwaka mmoja ikiwa  ni shamrashamra za miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Znzibar.hafla iliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Utalii Kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Saleh Yussuf Mnemo  akiuliza suali kwa Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni  na Michezo Mh.Tabia Maulid Mwita (hayumo pichani) kuhusu mchezo wa ngumi mara baada ya kuwasilisha taarifa ya mafanikio ya Wizara hiyo huko Ukumbi wa Wizara ya Utalii Kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya habari Maelezo Zanzibar Hassan Khatibu Hassan akiuliza suali kwa Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni  na Michezo Mh.TABIA Maulid Mwita (hayupo pichani) kuhusu taarabu katika maadhimisho ya mapinduzi mara baada ya kuwasilisha taarifa ya mafanikio ya Wizara hiyo huko Ukumbi wa Wizara ya Utalii Kikwajuni Zanzibar.

Picha na Fauzia Mussa - Maelezo Zanzibar.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.