Habari za Punde

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Asaini Hati ya Makabidhiano ya Msaada Kutoka IOM.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui (katikati) akisaini  hati ya makabidhiano ya msaada wa vifaa  mbalimbali  kwa ajili ya matumizi katika nyumba salama, wapili kutoka kushota ni Mwakilishi Mkaazi  kutoka Shirika la  Umoja wa Mataifa la Uhamiaji  IOM Nchini Tanzania Dk.  Qassim Sufi nae akisaini hati hiyo, makabidhiano hayo yalifanyika Ukumbi wa nyumba za kuhifadhia  Wazee Welezo.

Na Khadija Khamis –Maelezo .

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui  amewataka wazazi na walezi kushirikiana na Serikali katika mapambano ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto  nchini .

Hayo ameyasema katika Nyumba ya kulelea Wazee, Welezo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya matumizi mbali mbali kwa ajili ya nyumba salama ya kuhifadhia wahanga wa udhalilishaji kutoka kwa Muakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji Nchini Tanzania  (IOM) Dr Qasim Sufi .

Amesema vitendo vya udhalilishaji ni janga la kitaifa hivyo iko haja jamii kiujumla kushirikiana kwa pamoja na Serikali ili kuhakikisha vitendo hivyo vinaondoka katika jamii .

Aidha ameitaka jamii kutokuwa na muhali wa kuwaficha wahalifu wa vitendo hivyo kufanya hivyo kutasaidia mapambano ya vita dhidi ya udhalilishaji .

“Ni wajibu wetu kushirikiana kwa pamoja kuunga mkono  mapambano ya vita dhidi ya udhalilishaji wa wanawake na watoto tuacheni muhali, tuwe mstari wa mbele kwa kutoa ushahidi wa ukweli .“alisema Waziri .

Nae Muakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji Nchini Tanzania  (IOM) Dr Qasim Sufi  amesema iko haja kusaidia nyumba salama hapa Zanzibar kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji .

Amesema tatizo hilo ni la kidunia ambalo limekuwa likiwaathiri hususan wanawake na watoto ambao wameonyesha kuathirika zaidi duniani kote.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee, Abdalla Saleh Omar amesema nyumba salama inapokea watoto waliofikwa na kadhia mbali mbali ikiwemo udhalilishaji wa kingono kama  kubakwa, kulawitiwa pamoja na kupigwa kupitiliza .

Pia amesema usafirishaji haramu wa  wahanga ambao hutumika kwa  kufanyakazi za majumbani wakiwa katika umri mdogo hupatia hifadhi ya muda watoto hao, ambapo kwa kipindi cha mwezi wa Agosti hadi Oktoba mwaka huu wahanga walipokelewa 22 katika nyumba salama  kwa hifadhi ya muda.

Hata hivyo alisema wahanga hao wa kike ni 19 na wa kiume ni 3 wengine hupelekwa  katika nyumba salama kwa shaka ya kudhurika ikiwa wazazi wakishtukiwa kuwa watumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na watoto waliokosa jamaa hapa Zanzibar.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jami,i Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui (wa kwanza kulia) na Mwakilishi Mkaazi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji  IOM  Dk. Qassim Sufi  wakionyesha hati  ya makabidhiano ya msaada wa vifaa mbalimbali walivyokabidhiana ikiwa ni msaada   kutoka Shirika la  Umoja wa Mataifa la Uhamiaji  IOM  mara baada ya kusaini hati hiyo huko Ukumbi wa nyumba za kuhifadhia  Wazee Welezo.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jami,i Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akiangalia baadhi ya vifaa kwaajili ya matumizi katika nyumba salama ikiwa ni msaada kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji  IOM  .
Baadhi ya vifaa walivyokabidhiwa Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji  IOM.
Mkurugenzi Idara ya Ustawi wa Jamii Abdalla Saleh Omar akizungumza  baada ya kuwasilisha ripoti ya nyumba salama kwa kipindi cha mwezi wa Agosti hadi Oktoba 2021, katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa Vifaa vya matumizi mbalimbali kwaajili ya Nyumba salama, kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji  IOM , huko Ukumbi wa Nyumba za kulelea Wazee Welezo Zanzibar.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya matumizi kwaajili ya  nyumba salama, kulia ni Naibu katibu mkuu Wizara ya afya  Bi. Abeda Rashid , kushoto ni Mwakilishi Mkaazi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji  IOM  Nchini Tanzania Dk. Qassim Sufi, makabidhiano hayo yalifanyika Ukumbi wa nyumba za kuhifadhia  Wazee Welezo.
Baadhi ya Watendaji wa Idara ya Ustawi wa Jamii wakifuatilia tukio la makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya  matumizi katika nyumba salama hafla iliyofanika Ukumbi wa nyumba za kuhifadhia  Wazee Welezo.

Waziri wa Afya Ustawi, wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mzrui (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Idara ya Ustawi wa jamii

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.