Habari za Punde

Dr Shein azindua Maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa CCM

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika Viwanja Vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, katika sherehe za ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.
Dk. Shein akivalishwa skafu baada ya kuwasili katika Viwanja Vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.
Viongozi mbalimbali wakimlaki Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili katika viwanja vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika tukio la Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika katika viwanja vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja
Vijana wa halaiki wakitumbuiza kwa nyimbo na kuandika mambo mbalimbali wakati wa sherehe za Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza kuwasilisha salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Katika sherehe za  Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika katika viwanja vya Mwehe Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndg Shaka Hamdu Shaka Akizungumza katika Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika katika viwanja vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwasilisha salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT), katika sherehe za Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwehe Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Ali Mohame Shein akizungumza wakati wa akizindua sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM.

                                   (PICHA ZOTE NA CCM MAKAO MAKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.