STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 05.01.2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliofariki
kutokana na ajali ya kuzama kwa boti huko Mkoa wa Kusini Pemba.
Katika salamu hizo
za rambirambi, Rais Dk. Mwinyi alieleza
kusikitishwa na vifo hivyo na kuzinasihi familia za marehemu hao kuwa na subira
na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.
Rais Dk. Mwinyi alimuomba
Mwenyezi Mungu awalaze Marehemu wote mahala pema peponi, Amin.
Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi
aliwaombea kwa MwenyeziMungu wale wote waliopata madhara kufuatia tukio hilo
kupona kwa haraka.
Ajali hiyo imetokea
jana jioni (04.01.2022) baada ya boti waliyokuwa wakisafiria wananchi hao kuelekea
msibani huko Kisiwa Panza wakitokea Chake Chake Pemba kuzama, ambapo kwa mujibu
wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor Masoud, vyombo vya
uokozi bado vitaendelea na taratibu za kuwatafuta waliofariki ama wale
walionusurika na ajali hiyo.
Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,
Ikulu Zanzibar
No comments:
Post a Comment