Na Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar. 28/01/2022
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Wawekezaji wanatarajia kuzifanyia matengenezo nyumba za Mji Mkongwe ili kuepusha athari ambazo zitajitokeza baadae.
Hayo ameyasema na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar Bi.Madina Haji Khamis wakati alipofanya ziara na Wajumbe wa Tume ya UNESCO huko Forodhani.
Amesema Serikali imeamua kutengeneza mfuko kutoka Mji Mkongwe na sheria imeshapitisha hivyo utasaidia kuondoa changamoto za majengo hayo.
Amesema suala la umiliki wa nyumba hizo ni la Idara ya Nyumba,Wakfu na wamiliki binafsi ikiwa Mamlaka ya Mji Mkongwe ni wasimamizi tu.
Akizungumzia Ujumbe wa Tume ya Unesco kufanya ziara katika MjiMkongwe amesema lengo ni kuona changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kuwasilisha ripoti mamlaka husika ili kuzifanyia kazi.
Nae Mshauri wa Sheria Tume ya Taifa Unesco ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Caroline Joseph amesema tume ya Unesco imeundwa ili kusimamia mikataba iliyoridhiwa na kuitekeleza.
Amesema kuhusu MjiMkongwe amesema Tume ya Unesco imeamuamua kuona mji huo inaingia katika urithi wa dunia.
No comments:
Post a Comment