Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ashiriki Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dodoma

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM Taifa ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, wakiwa katika ukumbi wa White House Dodoma, kabla ya kuanza kwa Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, kilichofanyika leo 8-2-2022.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakisoma makabrasha kabla ya kuaza kwa Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) (wa kwanza kulia) Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Dkt.Philip Mpango, Mjumbe wa Kamatin Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Kassim Majaliwa.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Kikao cha Kamati Kuu ya Hamashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM) wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa White House wakati wa kuwasili kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. Kilichofanyika leo 8-2-2022 Jijini Dodoma.(Picha na Ikulu)  
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM Taifa, kilichofanyika katika ukumbi wa White House Jijini Dodoma leo 8-2-2022.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.