Habari za Punde

Imeonekana Kuna Changamoto Katika Suala Zima la Takwimu za Wanawake Wanaoshiriki Katika Nafasi za Uongozi.

Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi.Mashavu Khamis Omar akizungumza na Maofisa wa TAMWA -Zanzibar na ZAFELA walipofika ofisini kwake leo kwa mazungumzo.

Baadhi ya Maafisa wa TAMWA-ZNZ na ZAFELA leo tarehe 16/5/2021 wamefika na kufanya mazungumza na Kaimu Mtakwimu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mashavu Khamis Omar.

Mazungumzo hayo yaliofanyika katika ofisi ya mtakwimu Mazizini mjini Unguja.

Mkutano huo wenye lengo   la kuongeza uhamasishaji wa utunzaji wa taarifa za kitakwimu kuhusu wanawake na uongozi ambapo bado imeonekana kuna changamoto katika suala zima la takwimu za wanawake wanaoshiriki katika nafasi za uongozi kwenye nafasi mbali mbali visiwani hapa.

Awali akiwasilisha taarifa ya        dhumuni la kikao hicho Afisa utafiti na tathmini kutoka TAMWA-ZNZ Mohamed Khatib alisema  kuwepo kwa takwimu sahihi    ambazo zitawaonesha idadi ya wanawake wanaoshika nafasi za uongozi  utaleta tija kubwa sambamba na kuwa na mipango bora ya kuhamasisha wanawake wengine zaidi kujitokeza.

Kitengo*cha *mawasiliano

TAMWA ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.