RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka waumini
wa Dini ya Kiislamu kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili aifanye dunia kuwa na
amani na kuondokana na changamoto za kiuchumi.
Alhaj Dk. Mwinyi ametoa wito huo katika nasaha alizozitoa kwa waumini walioshirki ibada ya Sala ya Ijumaa, iliofanyika Masjid Shura Umbuji, Mkoa Kusini Unguja.
Amesema vita vinavyoendelea kati ya Russia na Ukrane, ugonjwa wa Covid-19, pamoja na upandaji wa bei ya Mafuta vimesababisha baadhi ya bidhaa muhimu kupanda bei na kupelekea athari kubwa za kiuchumi Dunia.
Aidha, aliwataka wananachi kuendeleza umoja na mshikamano kwa kigezo kuwa mambo hayo huleta amani na kuwa chachu ya maendeleo.
Alieleza kuwa katika hali ilivyo hivi sasa, jamii haizingatii umuhimu wa mambo hayo kwa vile nchi iko katika hali ya amani.
Sambamba na hayo, Alhaj Mwinyi alisisitiza umuhimu wa wananchi kufanya kazi kwa bidii katika kujitafutia maendeleo.
Katika hatua nyengine, Alhaj Dk. Mwinyi amepokea maombi ya wananchi wa Umbuji ya kusaidia upatikanaji wa Zulia, Kipaza sauti pamoja na matengenezo ya Mnara wa Maji wa Masjid Shura.
Nae, Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwataka waumini hao kuendelea kumuombea Dua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Mwinyi, ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Mapema, Khatibu katika Sala hiyo ya
Ijumaa Sheikh Idd Mrisho Vuai aliwataka waumini kuzingatia umuhimu wa
kushikamana, kupendana na kushirikiana,
ak kuepuka chuki, bughudha na
ugomvi, sambamba na kusistiza haja
kushikamana na mafunzo ya Mtume Muhamad (SAW).
Wakati huo huo, Rais Alhaj Dk. Mwinyi alipata fursa ya kufika nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Amani Mussa Hassan kwa jili ya kutoa mkono wa pole kutokana na kifo cha Baba yake mzazi.
Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano
Ikulu Zanzibar.
No comments:
Post a Comment