Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Wilaya ya Magharibi "A" Unguja.

Muonekano wa Jengo la Hospitali ya Wilaya ya Magharibi "A" Unguja lililojengwa kwa Fedha za Covid -19, katika eneo la Mbuzini katika Wilaya hiyo lililowekwa Jiwe la Msingi la ujenzi wake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakati wa ziara yake kutembelea Miradi ya Mendeleo Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea jengo jipya la Hospitali ya Wilaya ya Magharibi "A" Unguja linalojengwa kupitia Fedha za Covid 19 jengo hilo linalojengwa katika Kijiji cha Mbuzini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Mwinyi aliweka jiwe la msingi katika hospitali mpya ya Wilaya, iliyopo Mbuzini, Wilaya ya Magharibi A, na kusema kwamba kuimarika kwa huduma za afya kunahitaji hospitali za rufaa kama hizo zinazojengwa na Serikali.

Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba maendeleo ya nchi yanahitaji kwa kiasi kikubwa huduma za afya pamoja na elimu na ndio maana Serikali anayoiongoza imeweka kipaumbe katika sekta hizo.

Pamoja na hayo, Rais Dk. Mwinyi aliwahakikishia wananchi kwamba Serikali anayoiongoza itahakikisha inafanya kazi ya kuimarisha huduma za jamii.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Amour Suleiman Mohammed alieleza kwamba hospitali hiyo imejengwa kwa fedha za mkopo kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambazo zina lengo la kuhuisha uchumi baada ya janga la UVIKO-19, ambapo ujenzi wake unafanywa na Kampuni ya CRJE kutoka China.

Alieleza kwamba ujenzi wa hospitali hiyo umetengewa TZS Bilioni 3.9 ambapo hadi kufikia sasa jumla ya TZS Bilioni 2.4 zimeshalipwa sawa na asilimia 62 ambapo hii sasa ujenzi huo tayari umeshafikaia asilimia 80 na unahusisha majengo yatakayoweza kutoa huduma tofauti za afya.

Alieleza huduma ambazo zitatolewa katika hospitali hiyo zikiwemo huduma za wagonjwa wa dharura, huduma za wagonjwa mahututi (ICU), huduma za wagonjwa wa ndani zikiwemo wodiza watoto chini ya mwezi mmoja, wodi ya watoto, mama wajawazito, watu wazima wanawake na wanaume, wodi ya wagonjwa wa maradhi ya kuambukiza na huduma nyengiezo.

Halikadhalika, Rais Dk. Mwinyi alipokea ombi la Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Mudrik Ramadhan Soraga la kujengwa barabara inayotoka Mndo hadi Kiboje Manzese.

Vilevile, Rais Dk. Mwinyi alitembelea mradi wa uhuishaji na uimarishaji wa mfumo wa maji safi Zanzibar ambao unajenwga na Kampuni Megar Ingeniaring kutoka India ambao thamani wa TZS Bilioni 27.8 utakaosaidia katika vijiji vya Dole, Kizimbani, Sharifumsa, Kizimbani, Bububu pamoja na maeneo mengine ya Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa mradi huo utamaliza sehemu kubwa ya tatizo la maji katika Mkoa wa Mjaini Magharibi ambapo matarajio ifikikapo mwaka 2025 upatikanaji wa maji kwa asilimia kuwba utaongezeka na kusisitiza kwamba mradi huo ni vyema ifikapo Januari unakamilika kwa wakati kama mkaba ulivyoainisha.

Katika hatua nyengine, Rais Dk. Mwinyi alitembea barabara ya Mwera hadi Kibondemzungu ambayo ni ya mfano inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa ni miongoni mwa baraara za ndani zenye urefu wa kilomita 275.9 zinazojengwa Unguja na Pemba.

Rais Dk. Mwinyi alisema hatua ya Serikiali ya kujenga barabara hizo kwa kiwango cha lami ni kuondokana na changamoto ya ujenzi wa barabara kwa kifusi na hatimae kuharibika wakati wa mvua.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa alitoa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Mkoa huo huko katika ukumbi wa Chuo cha Utalii, Maruhubi na kueleza mafanikio pamoja na changamoto za Mkoa huo.

Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano,

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.