MAFUNDI wa Kampuni ya Simba Developers Ltd
inayojenga Tangi la Maji Safi na Salama katika eneo la Sizini Kilindini Wilaya ya Micheweni Pemba wakiendelea na Ujenzi wa Tangi hilo.kama wanavyoonekana pichani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwasili katika eneo la Sizini Kilindini kukagua Ujenzi wa Tangi la Maji Safi na Salama, linalojengwa katika eneo hilo kupitia Fedha za Uviko-19, akiendelea na ziara yake Mkoa wa Kaskazini Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi
wakimsikiliza Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) akitowa maelezo ya
kiufundi ya Ujenzi wa Tangi la Maji la Sizini Kilindini Wilaya ya Micheweni
Pemba, akiwa katika ziara yake Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza na Wananchi wa
Kijiji cha Sizini Kilindini Wilaya ya Micheweni Pemba baada ya kuweka Jiwe la
Msingi la Ujenzi wa Tangi la Maji Safi na Salama, akiendelea na ziara yake
kutembelea Miradi ya Maendeleo
WANANCHI wa Kijiji cha Sizini Kilindini Wilaya
ya Micheweni Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akiwahutubia baada ya
kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Tangi la Maji.
MAFUNDI wa Kampuni ya Simba Developers
inayojenga Tangi la Maji Sizini Kilindini Wilaya ya Micheweni Pemba
wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza na Wananchi wa Kijiji
hicho wakati wa ziara yake kutembelea ujenzi wa Tangi hilo.
No comments:
Post a Comment