Habari za Punde

TEHAMA Kutasaidia Serikali Kujua Uwezo wa Watendaji Wao.

Na Kijakazi Abdalla.  Maelezo 18/07/2022

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupitia Wakala wa Serikali Mtandao  imesema kufanyika kwa tathmin ya watendaji wa TEHAMA kutasaidia serikali kujuwa uwezo wa watendaji wao ili kuendana na mabadiliko ya dunia.


Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Said Seif Said. ameyasema Hayo huko Skuli ya Kiembesamaki wakati akifungua zoezi la kufanyiwa tathmin kwa watendaji wa serikali, amesema hatua hiyo itawezesha utoaji wa huduma bora ikiwa pamoja na udhibiti wa rushwa na mapato ya serikali..

Amesema Serikali imeamua kufanya zoezi hilo ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ya ulimwengu ambayo itasaidia kuwatambua watendaji hao na uwezo wao.

 

Nae  Mkuu wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka chuo Cha Taifa SUZA Dk Abubakar Diwani Bakar amesema  kufanyika kwa tathmini hiyo kutasaidia kwenda sambamba na dhana nzima ya uchumi wa Buluu kwa maendeleo endelevu kwa  ustawi wa wananchi wake.

 

 

Nao bàadhi wa watendaji kutoka Wizara tofauti za serikali waliofanyiwa tathmini hiyo wamesema kwa kiasi kikubwa itawasaidia kutambulika kwao na utendaji wao wa kazi.

 

Zoezi hili la siku tano litawashirikisha watendaji wote wa  kitengo cha Tehama katika Wizara ,Mashirika na sekta nyengine za serikali za Mapinduzi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.