Habari za Punde

Hafla ya makabidhiano ya Ofisi ya Rais Ikulu leo

ALIYEKUWA Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Ikulu Zanzibar  Ndg. Mussa Haji Ali akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Ofisi ya Rais - Ikulu  wakati wa hafla ya kukabidhi Ofisi kwa Katibu Mkuu Mpya wa Ofisi ya Rais - Ikulu Zanzibar Ndg. Masoud Hussein Iddi (kulia kwake) makabidhiano hayo yaliyofanyika leo 9-8-2022. Katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais –Ikulu Zanzibar (Picha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu Zanzibar Ndg.Masoud Hussein Iddi akizungumza na Wakuu wa Idara za Ofisi ya Rais Ikulu, wakati wa hafla ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Katika Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Ndg. Mussa Haji Ali.(hayupo pichani) makabidhiano hayo yaliyofanyika leo 9-8-2022. Katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Rais - Ikulu Zanzibar  (Picha na Ikulu)
ALIYEKUWA Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Ikulu Zanzibar Ndg. Mussa Haji Ali akimkabidhi vitendea Kazi Katibu Mkuu Mpya wa Ofisi ya Rais –Ikulu Zanzibar  Ndg.Masoud Hussein Iddi (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Rais - Ikulu leo 9-8-2022.(Picha na Ikulu) 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.