Habari za Punde

Mutungi atakiwa kuingilia kati kuwanyanyua wanawake katika nafasi za uongozi

Meneja miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed (katikati)akizungumza na mratib mradi wa kuwawezesha wanawake kuwa viongozi (SWIL) Maryam Ame (kushoto) pamoja na Salma Moulid.
Mratib mradi wa kuwawezesha wanawake kuwa viongozi Zanzibar ( SWIL ) Maryam Ame akizungumza na washiriki wa makutano wa majadiliano ya siku moja
Baadhi ya washiriki wakiendelea na kazi za makundi kabla ya kuwasilisha sababu wanazoamini zinawakwamisha wanawake wengi Zanzibar kutokua viongozi.

Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ


TAMWA-ZNZ yamtaka msajili wa vyama vya siasa Nchini kuingilia kati ili  wanawake wengi zaidi waweze kuwa viongozi  Z’bar.


Chama cha Waandishi wa habari wanawake TAMWA-ZNZ kimemtaka Msajili wa vyama vya siasa Nchini Tanzania Jaji Francis  S. Mutungi kuangalia utaratibu utakaovitaka  vyama vya siasa Nchini kubadili vipengele vya katiba za vyama vyao ili kuleta usawa katika nafasi mbali mbali za uongozi kuanzia kwenye Chama hadi wale wanaopata nafasi kupitia uwakilishi wa maeneo yao kupitia vyama vyao.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Chama hicho Dkt Mzuri Issa,Meneja miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed alisema licha ya jitihada mbali mbali zinazoendelea kufanywa na wanaharakati bado wanawake wengi wameshindwa kufikia malengo ya kupata nafasi za uongozi.


Wakati akifungua mkutano wa majadiliano ya siku moja uliofanyika Tunguu Wilaya ya kati Unguja na kuwashirikisha  wadau kutoka asasi mbali mbali wenye lengo la kutazama kwa pamoja changamoto za kikatiba za vyama vya siasa ambazo inaaminika kuwa zimekua miongoni mwa  sababu kubwa ya inayowafanya wanawake kushindwa kutumiza malengo yao. 


Alisema ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi ni jambo ambalo limekua likisemewa kwa muda mrefu bila ya mabadiliko yanayoridhisha na  anadhani kuwa kitu pekee kilichobaki ni msajili kuvilazimisha vyama vyote Nchini kubadili vuipengele kwenye katiba zao.


‘’Naamini iwapo katiba zote za  vyama vya siasa vitaweka wazi ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi litakua suala la lazima na  ni wazi kuwa kilio cha wanawake cha muda mrefu kitamalizika na hatimae wanawake wengi zaidi watashika hatamu za uongozi’’aliongezea.


Wakichangia katika mkutano huo baadhi ya washiriki walisema zipo changamoto nyingi ukitoa madhaifu ya katiba za vyama vya siasa ambazo wanawake wamekua wakikutana nazo kila leo.


Mmoja miongoni mwao Mohamed Jabir alisema kutoka na mazingira yaliopo sasa inawalazimu wanawake wanaotaka kushika nafasi za uongozi kujiongeza zaidi kielimu na kuacha hofu.


Alisema kumekua na hofu kubwa inayowakabili  wanawake wengi wasomi wamekua wakihofia mazingira ya kazi zao au kusubiri kwa muda mrefu huku wakikosa ajira iwapo wataamua kuingia kwenye siasa za vyama vya upinzani.


‘’Nina wasiwasi mkubwa hwenda wasomi wengi wataendelea kushindwa kuingia kwenye siasa kutokana na mazingira kutokua rafiki wengi wao wana hofu kubwa’’aliongezea.


Sambamba na uwepo wa chanagamoto hizo alisema bado wanawake wana fursa za kuwa viongozi na hawapaswi kukatishwa tamaa na vikwazo vya aina hiyo.


Nae Hawra Shamte alisema ili wanawake wengi waweze kushika nafasi kuna haja kila mmoja kuona suala la wanawake si jambo ambalo linapaswa kuwa wanaume pekee badala yake ni haki ya msingi ya kila mtu mwenye akili timamu.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.