Na Mwashungi Tahir- Maelezo 02/08/2022
Vyama vya siasa Zanzibar vimetangaza rasmin kushiriki katika Sensa ya Watu na Makaazi ifikapo tarehe 23 Ogasti 2022.
Wakizungumza katika Mkutano maalum uliofanyika katika ukumbi wa Takwimu Mazizini wamesema ili serikali iweze kupanga mipango yake kwa usahihi ya kuwaletea Wananchi maendeleo ,ni vyema kuungana pamoja katika kuhesabiwa ili ipatikane idadi kamili
Wamesema sensa haihusiani na siasa Bali ni mhimili wa maendeleo ya Taifa hivyo ni vyema kwa wanachama nao wakaashiriki kutoa taarifa sahihi wakati karani wa sensa atakapofika katika nyumba zao .
Aidha wamesema itikadi zao za kisiasa kwa sasa zimeweka kipaumbele maslahi ya taifa kwa lengo la kuipa nguvu serikali katika kupanga mipango yake ya kiuchumi ya miaka kumi ijayo Kama yalivyo malengo endelevu ya mkakati wa Dunia.
Sensa ya mwanzo ilifanyika nchini katika mwaka 1967 ikiwa moja ya mataka ya kimataifa kuhakikisha Serikali inaandaa, kupima na kutathmini utekelezaji wa maendeleo yake
No comments:
Post a Comment