Habari za Punde

TAMWA yataka muswada wa sheria kusimamia mambo yanayohusiana na dini

Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar University Dkt,Sikujua Omar Hamdani alipokua akiwasilisha ripoti ya awali kuhusu changamoto hizo.
Sheikh Nassor Tajo akichangia katika mkutano huo ambapo alisema ni muhimu kuwepo kwa sheria hiyo kwa kuwa itaondoa changamoto nyingi katika jamii.

Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano huo mara baada ya kujadili ripoti ya awali ilioleza changamoto za kukosekana sheri maalumu ya kusimamia mambo yote yanayohusikana na uislamu.


Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ

Chama cha waandishi wa habari Wanawake TAMWA-ZNZ kimesema wakati umefika kwa Zanzibar kuwepo kwa sheria maalumu itakayosimamia baadhi ya maswala yanayohusu dini ya kiislamu ikiwemo ndoa, talaka, mirathi, haki za wanawake pamoja na matunzo ya watoto ambao wazazi wameachana.

Akifungua mkutano wa siku moja uliowashirikisha wadau wa taasisi mbali mbali pamoja na viongozi wa dini mkuu wa miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed alisema kwa miaka mingi Zanzibar licha ya kuwa na idadi kubwa ya waislamu lakini imekosa sheria hiyo ambayo wanaamini kukosekana kwake kunaleta changamoto kubwa ikiwemo baadhi ya wahusika kutowajibika ipasavyo katika majukumu yao ya kila siku.

Alisema kutokuepo kwa sheria hiyo imesababisha maswala mengi yanayohusu dini ya kiislamu kuwa na mkanganyiko mkubwa kutokana na tofauti zinazojitokeza wakati wa maamuzi kutoka kwa watu wanaowaamini ikiwemo makaadhi na maulamaa.

Alieleza kuwa ili changamoto hiyo iweze kuondoka ni lazima kuwe na sheria maalumu ambayo itaelekeza na kusimamia kila kitu namna ya utekelezaji kuhusu uislamu.

Akitolea mfano alisema baadhi ya wanawake wanaoachika wamekua wakikutana na changamoto kubwa ya kukosa matunzo yao na watoto wao jambo ambalo dini imeweka wazi namna ya kuwatunza watoto hata kama wazazi wameachana.

Sambamba na hayo akifafanua zaidi pia suala la mirathi kwa familia ambazo wazazi wao wamefariki baadhi ya ndugu zao huamua kufanya wanachoamini wao ni sawa na iwapo imetokea mmoja kuwa na ugonjwa wa akili huwa hawi sehemu ya wanaopewa mirathi au mali yake hutumiwa na wengine bila yeye kunufaika.

Akiwasilisha ripoti ya awali baada ya kuzipitia sheria mbali mbali za kiislamu Zanzibar Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Zanzibar University Dkt,Sikujua Omar Hamdan alisema wakati anapitia sheria hizo aligundua changamoto ambazo anaamini zikifanyiwa kazi Zanzibar itapiga hatua zaidi.

Kwa nyakati tofauti wakichangia katika mkutano huo baadhi ya wajumbe walisema suala la uwepo wa sheria lilipaswa kufanyiwa kazi kwa miaka mingi lakini inasikitisha hadi sasa licha ya uhitaji wa sheria hiyo wenye mamalaka hawajalipa umuhimu jambo hilo.

Mmoja miongoni mwao Sheikh Nassor Tajo kutoka ofisi ya Mufti Zanzibar alisema sheria ya kadhi haikupaswa kubebeshwa maswala ya mtoto au yoyote yale yanayohusiana na maswala ya kiislamu isipokua sheria hiyo ipo kwa ajili ya kuanzishwa mahkama ya kadhi na kutoa mamlaka ya mahakama hiyo.

Alisema TAMWA-ZNZ wamekuja na wazo muafaka na wakati sahihi ambapo iwapo sheria hiyo itapatikana itaipunguzia mzigo mahkama ya kaadhi usiokua walazima.

Nae Mwenyekiti wa Jumuia ya watu wenye ulemavu Zanzibar (JUWAUZA)  Bi Salma Sadat alisema iwapo sheria hiyo itapitishwa itakua sheria nzuri na italeta msaada mkubwa kwa jamii.

Hata hivyo alisema lakuzingatia zaidi ni kuingiza vipengele kwenye sheria hiyo vitakavyohusisha watu wenye ulemavu ukizingatia kumekua na matukio mengi ya wanawake kutelekezwa kwa sababu ya kuzaa watoto wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.