Habari za Punde

Ufunguzi wa Kongamano la Wajasiriamali lililoandaliwa na Taasisi ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar

Wajasiriamali na Washiriki wa Kongamano la Wajasiriamali wakimskiliza kwa makini Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo uliofanyika Ukumbi wa CCM Amani Mkoa.
Mwenyekiti wa Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tawhida Cassian Galos akieleza kuhusu Kongamano la Wajasiriamali wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo  ambapo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Nane kwa kutega Fedha nyingi kwa Mikopo ya Wajasiriamali N

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza na Wajasirimalai walioshiriki Kongamanao lililoandaliwa na Taasisi ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar wakati akizindua Kongamano hilo lililofanyika Ukumbi wa CCM Mkoa Amani Zanzibar ambapo amewataka Washiriki hao kutumia Fursa za Mikopo nafuu zilizowekwa na Rais Dkt. Mwinyi ili kuweza kujikwamua na Umaskini

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa pamoja na Vikundi mbali mbali vya wajasiriamali ili kuweza kuzifikia Fursa zilizopo Nchini kwa kuwainua Wananchi wake.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa Kauli hiyo kwenye Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid katika ufunguzi wa Kongamano la Wajasiriamali lililoandaliwa na Taasisi ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) lililofanyika Ukumbi wa CCM Mkoa Amani.

 

Amesema Serikali imeanzisha Programu Maalum ya kuimarisha Uwezeshaji Wananchi kwa Lengo la kutoa Fursa za Ajira kwa kuwawekea Mazingira mazuri pamoja na kuwajengea uwezo Vijana na Wanawake ili kupunguza Umasikini Nchini.

 

Amesema Serikali imeanzisha ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Kulea na Kukuza Wajasiriamali Nchini, Mradi wa Ujenzi wa Vituo vya Kutoa Huduma za Ujasiriamali na Biashara pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Wajasiriamali.

 

Pamoja na hayo ameeleza kuwa Serikali imejipanga kujenga Masoko ya Kisasa ambayo yatatoa nafasi kwa Wajasiriamali kuweza kufanya Shughuli zao za Kiuchumi pamoja na kuchangamkia Fursa za kuuza Bidhaa wanazozalisha katika Soko la Ndani na Nje ya Nchi.

 

Aidha ameeleza kuwa Kupitia Fedha za Ahueni ya Uviko 19 Serikali ilitenga Jumla ya Shilingi Bilioni 31.6 za Kitanzania kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi kupata Mikopo yenye Gaharama nafuu, Boti na Vifaa mbali mbali vya kuendesha Shughuli zao.

 

Sambamba na hayo amewapongeza Washiriki wa Kongamano hilo kwa kupata Fursa hiyo ambapo amewataka kuwa makini ili kufikia lengo lililokusudiwa na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa nao na kutatua changamoto zitakazowakabili.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) Mhe. Tawhida Cassian Galos ameeleza kuwa Taasisi yao imeanzishwa kwa lengo la kuunga Mkono Juhudi za Serikali ambapo kuandaa Kongamano hilo kupitia Mashirika mbali mbali ni kuweza kuwasaidia Wajasiriamali wa Zanzibar.

 

Aidha ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kutenga Fedha nyingi za Mikopo Nafuu kwa ajili ya Wajasiriamali ambapo Mikopo hiyo itaweza kuwainua Wanawake pamoja na Vijana.

Kongamano hilo la Wajasiriamali limeandaliwa na Taasisi ya Rafiki wa Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWWAZA) kwa uafadhili wa  CRDB,NMB, ZRB pamoja VIGOR Group.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.