Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na IGP Wambura Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP.Camillus Mongoso Wambura, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-9-2022 kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP.Camillus Mongoso Wambura, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 13-9-2022 na (kulia kwake) Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar.CP.Hamad Khamis Hamad
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Mongoso Wambura, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-9-2022
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la   Mapinduzi  Dk. Hussein Mwinyi amesema Serikali itatoa kila aina ya msaada kuhakikisha Jeshi la Polisi linatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.

Dk. Mwinyi amesema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Mongoso Wambura, ambapo pamoja na mambo mengine amefika kwa ajili ya kujitambulisha.

Amesema Serikali inatambua uwepo wa changamoto mbali mbali zinazolikabili Jeshi hilo, hivyo akabainisha azma ya Serikali katika kuzitafutia ufumbuzi ili kuliwezesha jeshi hilo kutekeleza vyema majukumu yake.

Alisema lengo la kuwepo vyombo mbali mbali vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Polisi  ni kuhakikisha kunakuwepo usalama wa kutosha hapa nchini, huku akibainisha ushirikiano kuwa ndio kichocheo cha kuleta ufanisi wa vyombo hivyo.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa Serikali inaridhishwa na utendaji kazi  wa Jeshi hilo na hivyo akasisitiza azma ya kuendeleza ushirikiano mkubwa uliopo kati  ya Serikali ya Mapinduzin ya Zanzibar na Jeshi hilo.

Rais Dk.  Mwinyi alitumia fursa hiyom kumpongeza IGP Wambura  kwa  uteuzi aliopata katika chombo hicho kikubwa na chenye umuhimu mkubwa katika usalama wa nchi.

Nae, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Mongoso Wambura alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, imekuwa katika juhudi kubwa ya kuipatia ufumbuzi changamoto ya upungufu wa vifaa na vitendea kazi muhimu vya Jeshi hilo, hususan katika nyanja ya usafiri.

Alisema pamoja na Serikali kutoa fedha za kutosha kwa Jeshi hilo kwa jili ya ununuzi wa Vifaa, lakini hivi karibuni imepokea msaada mkubwa wa magari 72, huku magari mngine 78 yakiwa njiani (katika meli) kuja nchini.

“Kuna magari mengine 117 yanaendelea na matengenezo kiwandani kwa ajili ya Jeshi letu  na mara tu yatakakamilika yataletwa hapa nchini”, alisema.

IGP Wambura alisema ugavi wa magari  hayo tayari umefanyika ambapo Jeshi la Polisi Zanzibar limepatiwa jumla ya magari kumi (10) kwa ajili ya Mikoa Mitano, Chuo cha Polisi Ziwani pamoja na Kikosi cha kutuliza ghasia ‘Field Force Unit’.

Aidha, alisema Mikoa hiyo pamoja na Mikoa mingine ya Tanzania Bara itaendelea kupatiwa magari hayo kadri yatakavyowasili hapa nchini.

Akigusia suala la kukosekana kwa usalama katika mipaka ya Zanzibar,  IGP Wambura alisema, kwa kuitikia agizo za Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu, Jeshi hilo linalifanyika kazi kikamilifu suala hilo kwa kuzingatia umuhimu wa usalama nchini.

Alisema kwa kuanzia wamefanya kikao muhimu kilichowashirikisha Maofisa wa Jeshi hilo kutoka pande mbili za Muungano ili kuabini chanzo cha tatizo hilo pamoja na kuzingatia uwepo wa rasilimali watu kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.