Mhe. Makamu ameyasema hayo huko hoteli ya Park Hyatt Shangani mjini Zanzibar, katika
hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji kati ya Marekani na Tanzania.
Amesema kutokana na dhamira hiyo, hivi sasa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imerahisisha taratibu za maombi ya uwekezaji na kwamba kibali kinaweza kupatikana ndani ya kipindi
kifupi cha kumuwezesha muwekezaji ama mfanyabiashara kuendelea na shughuli zake
za kibishara kwa wepesi.
Mhe. Othman amefahamisha kwamba kongamano hilo linalojumisha wataalamu, kutoka nchi tofauti ikiwemo Kenye, Afrika
Kusini , Tanzania na Marekani ni muhimu kwani wataweza kujadili changamoto
zilizpo na kupendekeza njia bora za kuzitatua ili kuleta maendeleo ya biashara
na uwekezaji Zanzibar.
Aidha Mhe. Othman amepongeza juhudi za rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hasan na Rais wa Zanzibar Mhe. Dk
Hussein kwa Juhudi zao za kuitaingaza nchi kiutalii kupitia filamu ya Royal
Tours iliyozinduliwa Marekani Mwezi Aprili mwaka huu wa 2022.
Amesema hatua hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa ndani ya
kipindi kifupi kujitokeza wawekezaji
wengi na kuongezeka uwekezaji wa kibiashara ndani ya Tanzania Bara na
Zanzibar ikiwa ni matokeo ya filamu hiyo.
Mhe. Othman ameongeza kwamba
juhudi hizo zimechangia kuwezesha
Tanzania hivi sasa kwa na jumla ya
Kampuni kubwa 19 za kibiashara kutoka
Marekani na wameweza kuwekeza kwa mtaji
wa kiasi cha dola trilioni 1.6.
Aidha amesema kwamba pia sera ya uchumi wa Buluu iliyoasisiwa
hapa Zanzibar inalenga kuzitumia vyema
fursa na rasilimali za baharini huku
ikiweka mazingatio makubwa katika suala la uhifadhi na usimamizi wa mazingira
yasichafuliwe.
Pia Mhe. Othman amesema kwamba Serikali imefanya marekebisho
ya sheria yake namba 14 ya mwaka 2018 ya Mamlaka ya Kuendeleza na Kukuza Vitega
Uchumi Zanzibar (ZIPA) na kulitenga eneo la Pemba kuwa ni maalumu kimkakati
katika uwekezaji.
Amefahamisha kwamba kutokana na hali hiyo sheria hiyo imeweka
vivutio maalum kwa wewekezaji wote watakaokwenda kuwekeza katika eneo la Kimkakati
la Micheweni Pemba na kwamba jambo hilo linania la kusaidia eneo hilo
kuendelezwa zaidi kibiashara.
Naye waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar ,
Omar Said Shaaban amesema kwamba serikali inafanya juhudi ili kuiwezesha sekta
ya maendeleo ya bishara kwenda sambamba
na mahitaji ya wataalamu wanaohitajika katika sekta hiyo.
Amesema ujio wa Kampuni zaidi ya 20 kutroka Marekani
zilizoshiriki katika Kongamano hilo ni hatua kubwa katika kukuza sekta ya
biashara na kuongeza fursa za upatikanaji wa ajira nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Ajira na
Uwekezaji, Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga, amesema kwamba mkutano huo ni
muhimu katika kuainisha fursa na changanoto zilizopo katika jitihada za kukuza
sekta hiyo nchini.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo cha Habari leo tarehe 28.09.2022.
No comments:
Post a Comment