Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Amjulia Hali Rais Mstaafu Alhaj Dkt.Salmini Amour Juma na Kushiriki Kisomo cha Hitma na Dua ya Kuwaombea Wazee

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea kumjulia hali Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Salimini Amour Juma  nyumbani kwake Kidombo ,baada ya kumaliza kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na Dua na Kisomo cha hitma kuwaombea Wazee wa Kidombo (kuliakwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman na Amini Salimin  Amour. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.,Hussein Ali Mwinyi akimsalimia Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Salim Amour Juma alipofika nyumbani kwake Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja kuhudhuria kisomo cha Hitma na Dua ya kuwaombea Wazee wa Kijiji cha Kidombo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman akimsalimia Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Salim Amour Juma alipofika nyumbani kwake Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja kuhudhuria kisomo cha Hitma na Dua ya kuwaombea Wazee wa Kijiji cha Kidombo 
Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Salmin Amour Juma akisoma dua baada ya kumaliza mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi alipofika nyumbani kwake Kidombo kuhudhuria hafla ya kisomo cha Dua na Hitma kuwaombea Wazee.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Bw.Amini Saliman Amour baada ya kumjulia hali Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Salimin Amour Juma, nyumbani kwake Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.