Habari za Punde

SHAKA: Vyama vya Siasa Njooni Tujenge Nchi,Rais Samia Suluhu Ameonesha Njia

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akiwsasalimia na kuzungumza na Wananchi katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Taifa mjini Kibondo akiwa katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Mkoani Kigoma. 
Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa mjini Kibondo wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Kigoma.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameanza uongozi vizuri kwa kuwaunganisha Watanzania, hivyo vyama vya siasa vya upinzani viungane nae kujenga nchi.

Amesema Rais Samia ameonesha dhamira ya dhati kuwaletea maendeleo Watanzania bila ya kujali Itikadi zao, ni vyema akaungwa mkono.

Ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2022 alipokaribishwa kusalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa mjini Kibondo akiwa katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Kigoma.

"Tunawashukuru kwa kuja kuona mambo mazuri, karibuni tuungane pamoja tuijenge nchi yetu, nchi ni moja na taifa ni moja , Rais Samia ameanza vizuri kutuunganisha Watanzania mbali na imani zetu na itikadi zetu lakini Tanzania ni moja," amesema.

Aidha, Shaka amewashukuru viongozi wa vyama rafiki walioshiriki mkutano huo kwa kumuunga mkono Rais Samia na kusema Sasa ni wakati wa kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuleta maendeleo.

Awali Shaka, amesema Rais Samia ni mwana CCM kindakindaki na mwanamendeleo thabiti aliyedhamiria kuleta maendeleo ya kweli.

Shaka amesema kuwa Rais Samia ameonyesha kwa vitendo uthunutu wa hali ya juu kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi.

"Niwahakikishie wana Kigoma na Watanzania, ajenda ya maendeleo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ipo katika mikono salama. Maendeleo na Samia Suluhu Hassan ni kama kulwa na doto," amesema.

Amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipaumbele chake cha kwanza ni maendeleo na hilo limedhihirishwa na mkataba ambao Rais Samia, wabunge na madiwani walikabidhiwa katika uchaguzi wa 2020.  @ccmtanzania 
@samia_suluhu_hassan 
@shakazulu36 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.