Habari za Punde

CCM yatoa pole kufuatia ajali ya ndege Bukoba

 Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kimepokea kwa mshituko na huzuni kubwa taarifa ya ajali ya ndege iliotokea (leo) Jumapili tarehe 6 Novemba 2022 Saa 2:35 asubuhi katika ziwa victoria hatua chache kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera.


Ajali hii imehusisha Ndege ya shirika la Ndege la Precision yenye usajili 5H -PWF iliokuwa imebeba abiria 39, marubani 2 na wahudumu 2 ikitokea Dar es Salaam kuelekea Bokoba.


Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatoa Pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu  Samia Suluhu Hassan, Shirika la Ndege la Precision, Ndugu, jamaa na watanzania wote waliofikwa na  Msiba huu wa kuondokewa na wapendwa wetu 19 Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote  mahala pema Peponi. Amiin


Vilevile Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawaombea Kupona haraka majeruhi wote 26 waliokolewa na kufikishwa katika hospitali ya Rufaa Mkoani Kagera.  Tunawaomba Watanzania  wote kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na masikitiko, huku vyombo vyetu vinavyohusika vikiendelea na hatua za uokoaji na uchunguzi wa ajali hii.

Mungu Ibariki Tanzaia.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu Halmshauri Kuu ya  CCM Taifa, Itikadi na  Uenezi,
06 Novemba 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.