Habari za Punde

Mahafali ya Tatu ya Shahada ya Kijeshi kwa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa kushirikiana na Chuo cha Uhasibu Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwa ajili Wimbo wa Taifa na Ule wa Afrika Mashariki kabla ya Kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724(Wanaume 635) (Wanawake 89) kwa Cheo cha Luteni Usu katika Sherehe zilizofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha tarehe 26 Novemba, 2022.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwatunuku Shahada ya Sayansi ya Kijeshi Wahitimu 109 kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) kwenye Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha tarehe 26 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Wahitimu wa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwenye Sherehe za Mahafali zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha tarehe 26 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa zawadi Wahitimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwenye Sherehe za Mahafali zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha tarehe 26 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Wanafunzi mara baada ya Kuwatunuku Kamisheni kwa Cheo cha Luteni Usu kwenye Sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha tarehe 26 Novemba, 2022.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.