Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mikutano mbalimbali ya COP27, Sharm El Sheikh nchini Misri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Botswana Mhe. Mokgweetsi Masisi katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri tarehe 08 Novemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika moja ya Mikutano ilioandaliwa na Benki ya Dunia kuhusu miradi mbalimbali ya Mazingira inayosaidia kupunguza hewa ukaa kwenye muendelezo wa COP 27 nchini Misri tarehe 08 Novemba, 2022. Mkutano huo ulioongozwa na Rais wa Benki ya Dunia David Malpass, pia umehudhuriwa na Rais wa Msumbiji Filipe Nyussi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Watanzania waliofika kutembelea Banda la Maonesho la Tanzania lililopo ndani ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh nchini Misri tarehe 08 Novemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mabalozi wa Mazingira wa Tanzania mara baada ya kutembelea Banda la Maonesho la Tanzania lililopo ndani ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri tarehe 08 Novemba, 2022.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.