Habari za Punde

Jumuiya ya Umoja wa kheri (JUWAKHE) yawapatia mafunzo ya stadi za maisha kwa wahitimu wa mwaka 2022

Afisa Kiungo Tumbatu kutoka katika Kitengo cha Maradhi Yasioambukiza katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja, Mariamu Mohamed Mtumwa akitoa mafunzo kuhusu na matumizi ya Tumbaku, Sigara  na Madawa ya Kulevya na madhara yake, kwa Wanafunzi wahitimu wa mwaka 2022 wa Kidatu cha Pili na cha nne  katika Skuli ya Sekondari Benbella yalioandaliwa na Jumuiya ya Mahajjat wa 2016 Zanzibar .

Baadhi ya Wanafunzi wahitimu wa mwaka 2022 wa Kidatu cha Pili na cha nne wakisikiliza mafunzo ya stadi za maisha kwa Afisa Ukimwi Afya ya Uzazi na dawa za kulevya Riziki Mohamed Juma ( hayupo Pichani ) huko Skuli ya Sekondari Benbella yalioandaliwa na Jumuiya ya Mahajjat wa  Zanzibar wa mwaka 2016.


Baadhi ya Wanafunzi wahitimu wa mwaka 2022 wa Kidatu cha Pili na cha nne wakisikiliza mafunzo ya stadi za maisha kwa Afisa Ukimwi Afya ya Uzazi na dawa za kulevya Riziki Mohamed Juma ( hayupo Pichani ) huko Skuli ya Sekondari Benbella yalioandaliwa na Jumuiya ya Mahajjat wa  Zanzibar wa mwaka 2016.

Picha na Khadija Khamis, Maelezo.


Na Khadija Khamis -Maelezo , 02/01/2023.

Afisa wa Ukimwi, Afya ya Uzazi na Dawa za Kulevya Riziki Mohamed Juma amewataka wanafunzi kujipangia malengo Yao ya baadae kwani kufanya hivyo kutasaidia kujilinda na vishawishi kujiamini kuwa na udhubutu pamoja na kukabiliana na mihemko

 

Hayo ameyasema Leo katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Benbella wakati wa mafunzo ya stadi za maisha kwa wanafunzi walimaliza mitihani yao ya kidatu cha pili na Cha nne yaliotolewa na Jumuiya ya Umoja wa kheri  (JUWAKHE) iliyoundwa na Mahujaji Wanawake wa mwaka 2016. (Zanzibar Hajj group.)

 

Amesema kuishi uraia baada ya kumaliza skuli  kunakuwa na changamoto nyingi hivyo ni vyema Vijana hao wakapata muongozo wa kidunia na akhera Ili kuweza kuachana na vishawishi vya anasa ,madawa ya kulevya na vigengi viovu..

 

Aidha aliwataka Vijana hao kujilinda na viungo vya uzazi Ili visipate madhara kwa kuziepuka tabia zote hatarishi jambo ambalo litasaidia kuwa na familia Bora hapo baadae'.

 

"Afya ya uzazi humjenga mtu kiimani kihisia kiakili pamoja na kujielewa hivyo Vijana mnapazwa kuvilinda visipate madhara kwa Wanawake na wanaume pia"alisema Afisa huyo. 

 

Nae Afisa Kitengo Tumbatu kutoka Kitengo Cha Maradhi Yasioambukiza Hospitali ya Mnazi mmoja Mariyam Mohamed Mtumwa amewataka Vijana hao kutojihusisha na matumizi yaTumbaku,uvutaji wa sigara, keki shisha na aina yeyote ya  dawa za kulevya kutokana na adhari zake kuongezeka siku hadi siku

 

Amesema katika mwaka 2021 takwimu imeonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa maradhi yasioambukiza hasa saratani za aina zote .na katika Hospitali ya Ocean Road wazanzibar wameongoza  jambo ambalo linaathiri Bajeti ya Wizara ya Afya.

 

Alifahamisha kuwa Vijana kula matunda na mbogamboga kwa wingi na uwanga kidogo pia wafanye mazowezi  Ili kuyayushe mafuta yaliomo mwilini kwao.

 

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kheri Hijjat Kurthumu Yussuf Hemed  amesema azma ya kuanzisha Jumuiya hiyo ni kuweza kuwasaidia watoto yatima na wenye mazingira magumu kwa kadiri ya uwezo Ili kuendeleza Yale Mambo ya Kheri ambayo wanatakiwa kuyatekeleza katika maisha yao kama uislamu unavyoelekeza .

 

Amesema kuwa pamoja na hayo pia wanamuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada zake anazozitekeleza za kuwalinda watoto Ili waweze kufikia ndoto zaidi

 

Nae Mwanafunzi aliyemaliza elimu yake ya kidatu Cha nne Skuli ya Sekondari ya Biashara Khadija Abasi Issa amesema anaishukuru Jumuiya hiyo kwa kuwapatia mafunzo ya stadi za maisha Ili kujua namna  ya kuishi uraiani kwa kuwa na Imani kwamba zile ndoto zao walizozitarajia zitafikia .

 

Nae Abdulazizi Iddi kutoka Skuli ya Sekondari ya Biashara amesema kuumaliza kwa mitihani ya kidatu Cha nne tayari dhamana zimeondoka kwa walimu wao  hivyo Iko haja ya kujilinda na vishawishi na kufuata mafunzo na maadili ya wazazi na walezi wao.

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.