Habari za Punde

Rais Mhe. Samia azindua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai nchini, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kabla ya kuzindua Tume ya kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai tarehe 31 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika Mhe. Mussa Azan Zungu, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Mhe. Eng. Hamadi Masauni, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Zena Said pamoja na Wajumbe wa Tume ya kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai nchini Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kuzindua Tume hiyo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai nchini Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue pamoja na Katibu wa  Sekretarieti ya Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari, 2023.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.