Habari za Punde

Benki ya CRDB yatoa msaada wa vitanda 10 kituo cha Afya Levolosi, jijini Arusha

 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Festo Dugange (watatu kulia) akipokea sehemu ya msaada wa vitanda 10 kwa ajili ya kituo cha afya cha Levolosi, kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Kafui (watatu kushoto) uliotolewa na Benki ya CRDB kwa uratibu wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo (wanne kulia). Msaada huo unaelekezwa moja kwa moja katika Wadi ya Wanawake katika kituo hicho cha Levolosi kilichopo jijini Arusha ili kupunbuza adha iliyokuwepo hapo awali ya kulala wawili katika  kitanda kimoja. Msaada huo unathamani ya shilingi Milioni sita.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Hargeney Chitukuro.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Festo Dugange akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa vitanda 10 kwa ajili ya kituo cha afya cha Levolosi, kilichopo jijini Arusha, uliotolewa na Benki ya CRDB, Vitanda hivyo vinathamani ya shilingi milioni sita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.