Habari za Punde

TAMWA-ZNZ yaanza mkakati mpya kushuka mashuleni kutoa elimu ya udhalilishaji

 
Zaidi ya wanafunzi 300 kutoka shule mbili za wilaya ya mjini Unguja leo wamepatiwa mafunzo ya kujikinga na kutambua viashiria vya udhalilishaji katika maisha yao ya kila siku.

Shule hizo ni Memon ya Stown Town na Bubu ambapo maafisa wa TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na mitandao ya kupinga udhalilishaji (GBV network) wamekuwa wakitoa elimu kwa wanafunzi hao kwa nyakati tofauti.

Wakati wakitoa elimu maafisa hao  wakiongozwa na afisa anashughulikia maswala ya udhalilishaji TAMWA-ZNZ Zaina  Salum amesema wameamua kuwafikia wanafunzi mashuleni kutokana na sababu mbali mbali.

Alisema kwa kipindi kirefu wamekua wakitoa elimu kupitia vyombo vya habari jambo ambalo wanadhani kuna wakati elimu hiyo haifiki kwa walio wengi na ndio maana kila leo matendo hayo yamekua yakifanyika.

"Unajua ukija huku field ndio haswa unakutana na watoto wenyewe ambao ndio wanaokumbwa na kadhia hii,na hatuna hakika kutokana na umri wao kuwa wanaskiliza redio au kusoma magazeti" aliongezea.

Pia aliwataka watoto hao kufanya vitu muhimu ambavyo wanapaswa kuvifanya sasa kutoka na umri wao ikiwemo kujikita zaidi katika elimu.

 Mwawakilishi kutoka mtandao wa kupinga udhalilishaji Huda Gharib aliwataka wanafunzi hao kuwa makini sambamba na kuepuka makundi ya watu wasiowaamini hata mitaani mwao.

Pia aliwataka wanafunzi hao kutoacha kabisa kuwa na aina ya marafiki wasiokua wa umri wao kwani wanajua mambo mengi zaidi hivyo wanaweza kuwashawishi.

Kwa nyakati tofauti watoto hao walioneshwa kuguswa na elimu hiyo na kueleza kuwa wanapaswa kuifanyia kazi.

Mmoja wao Saida Awadhi aliwataka watoto wenzake kutoa taarifa kwa wazazi wao pale wanapoona mazingira hatarishi kwao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.