MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema Wanawake wengine wamekuwa ni sehemu kuwa katika kutoa mchango wa kuleta mabdiliko ya maendeleo kwa muda mrefu katika sekta na maeneo mbali mbali hapa Zanzibar kwa miaka mingi sasa.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko
Ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na timu ya Utunzi wa Kitabu cha Mchango wa wanawake kinachoitwa ‘Nyayo za
Wananwake Zanzibar’, iliyoongozwa na Meneja wa Mradi wa Uandishi wa Kitabu hicho Bibi Hannah MacCarriok kutoka
Sweeden.
Amesema kwamba hapa Zanzibar ipo mifano kadhaa wa kadhaa
inayoonesha mchango mkubwa uliotolewa na wanawake katika maeneo na mambo tofauti
ambao umechangia kuleta manufaa na maslahi makubwa kwa jamii jambo ambalo
linaonesha uwezo na umahiri walionao wanawake wengi nchini .
Amesema kuwepo mchanganyiko wa
maisha na utamaduni wa watu kutoka
makabila tofauti hapa Zanzibar imesaidia sana wanawake kutoa mchango wao katika
harakati za kupatikana haki na maendeleo kwa jamii kwennye Nyanja tofauti.
Mhe. Othman amefahamisha kwamba jamii
inapaswa ifahamu kwamba maendeleo bora ya familia yanahitaji kuwepo wanawake
mahiri, kwa kuwa ni wenye uthubutu na wanaweza kujenga ushawishi katika kubuni
na kutekeleza makakati na mipango
tiofauti ya maendeleo yao na jamii kwa jumla.
Amewapongeza washiriki wa Utunzi wa
Kitabu hicho ambacho kimechukua muda wa miaka mitatu kukamilika na kueleza
kwamba wamesaidia kuionesha jamii juu ya
suala kubwa la mchango wa wanawake katika maeneo mbali mbali.
Mhe. Othman amewataka watunzi hao
kuangalia maeneo zaidi ili kupanua wigo mpana katika kukifanyia mapitio na
hatua ya utoaji wa toleo la pili la kitabu hicho ili kuongeza mambo mengi zaidi
ya mchango wa wanawake yatakayoanishwa kwenye kitabu hicho.
Naye Meneja wa Mradi wa Utunzi na
uandikaji wa kitabu hicho Bibi Hannah MacCarriok, amesema kwamba mchango wa
mabadiliko katika jamii unaweza kufanywa na wanawake kutoka katika ngazi zote
ndani ya jamii.
Aidha amesema kwamba kitabu hicho
mbali na kuonesha machango wa wanawake mbali mbali, lakini pia kinalenga
kuonesha na kuwashajiisha wananawake katika kuwajengea uwezo na uthubutu wa
kushiriki katika masuala mbali mbali muhimu kwa maendeleo yao na taifa kwa
jumla kama walivyofanya wengine.
Mwisho.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo tarehe
02.02.2023.
No comments:
Post a Comment