Habari za Punde

MBUNGE UMMY AWAPA POLE WAATHIRIKA WA MVUA MAKORORA TANGA

 

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya katikati akimuonyesha kitu Afisa Mazingira wa Jiji la Tanga Kizito Mkwambi wakati alipofanya ziara kuangalia athari za mafuriko iliyotokana na mvua.

Na Oscar Assenga,Tanga. 

Mbunge wa Tanga Mhe Ummy Mwalimu leo tarehe 23/4/2023 akiambatana na Afisa Mazingira wa Jiji la Tanga,  Kizito Mkwambi amekagua baadhi ya miundombinu iliyoathirika na mafuriko jijini Tanga, ikiwemo eneo la Ziwani, Kata ya Usagara na Mzingani. 

Mhe Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya amelitaka Jiji na Tarura Wilaya ya Tanga kuangalia namna ya kuzibua mirefeji iliyoziba haraka ili kuondoa kero ya mafuriko eneo hilo na maeneo mengine ya Jiji. 

Aidha Mhe Ummy ameeleza kuwa Suluhisho la kudumu la kuondoa kero sugu ya mafuriko eneo la Ziwani ni kutafuta fedha ili kuchimba mfereji wa kupitisha maji yanayotuama katika eneo hilo. 

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya katikati akimsikiliza Afisa Mazingira wa Jiji la Tanga Kizito Mkwambi kulia wakati alipofanya ziara kuangalia athari za mafuriko iliyotokana na mvua


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.