MUONEKANO
wa Jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Kidongochekundi Wilaya ya Mjini Unguja lililojengwa
kwa fedha za Uviko -19.,. lililofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni shamrashamra za
kuadhimisha Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiondoa pazia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela
Mohamed Mussa, kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya
Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo 24-4-2023, na (kushoto kwa Rais)
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ikiwa ni
shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema
miaka 59 ya Muungano wa Tanzania imeleta Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya
Elimu kwa pande zote ikiwemo kuboresha miundombinu ya majengo ya kisasa na
huduma zenye ubora katika kutoa ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye sherehe za ufunguzi wa
Skuli ya msingi ya kisasa Kidongochekundu iliopo kwenye jimbo la Jang’ombe,
Wilaya ya Mjini ikiwa ni shamrashamra za miaka 59 ya Muungano wa Tanzania.
Alisema, Zanzibar kwasasa inastahiki kuwa na skuli za
msingi za ghorofa zenye ubora wa hali ya juu ili kuendana na hadhi ya miaka 59
ya Muungano wa Tanzania ambapo Serikali zote mbili ya Muungano wa Tanzania na
ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeshuhudia ongozeko kubwa la taasisi nyingi za elimu
na wanafunzi wengi.
Alisema, kabla ya Muungano wa Tanzania, sekta ya elimu
ilikua na wanafunzi 25, 000 na sasa idadi imeongezeka kufikia 570,000.
Akizungumzia miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais Dk.
Mwinyi alisema Serikali ina mpango wa kuongeza madarasa 1000 yenye miundombinu
na vifaa vya kisasa zikiwemo maabara, vyumba vya kompyuta, maktaba, vyoo vya
kisasa na ofisi za walimu pamoja na kufungua miradi mikubwa zaidi ya maendeleo.
Alisema mabadiliko ya elimu Zanzibar yatafikiwa kwa kuwa
na ujenzi imara wa miundominu ya majengo ya kisasa yatakayochukua wanafunzi
wachache kwenye madarasa, vifaa vya kisasa na mazingira mazuri ya kufundisha na
kujinza.
Rais Dk. Mwinyi aliongeza skuli ya Kidongochekundu Msingi
ni miongoni mwa mfano hai wa skuli zote za msingi anazotaka kuzijenga Zanzibar
hadi kufikia Januari, 2025 pamoja na kukamilisha miradi mengine mikubwa ya
maendeleo ili kuendana sambamba na hadhi ya miaka ya Mapinduzi ya Zanzibar na
miaka 59 ya Muungano wa Tanzania.
“Skuli hii ni mfano wa skuli zetu za msingi nnazotaka
ziwe nchini, skuli za ghorofa ambazo ndani yake mna maabara za sayansi,
maktaba, vyumba vya kompyuta na madarasa wanafunzi wetu wasiozidi 45” alielekeza
Dk. Mwinyi
Alisema serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha
Zanzibar inapata madarasa ya kutosha, nyenzo bora za kusomea ikiwemo
kufanikisha skuli kuwa na mkondo mmoja badaya ya miwili kama awali. Aidha,
aliwataka watendaji wa wizara ya elimu kuhakikisha skuli inatoa huduma
zinazoendana na hadhi yake kwa kutoa ufaulu mzuri kwa wanafunzi.
Naye, Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Amali, Lela
Mohamed Mussa alisema ujenzi wa skuli hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi
ya 2020/2025 ambapo serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar iliahidi kujenga miradi
malimbali ya maendeleo.
Alieleza Wizara ya Elimu imepiga
hatua kubwa katika kukamilisha miradi yote iliyopanga na kwamba imeakisi dhima
ya miaka 59 ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu Mkuu wizara ya
Elimu, Khamis Said alisema ujenzi wa skuli hiyo umegharimu shilingi bilioni
4.466 ambao umejumuisha Maktaba, Maabara, chumba cha kompyuta, ofisi ya mwalimu
kuu, ofisi ya msaidizi mwalimu mkuu, ofisi tatu za walimu, chumba cha kusalia,
vyoo 25 , viti na meza 1305 kwaajili ya wanafunzi wote.
Skuli ya Msingi Kidongochekundu ni miongoni mwa skuli
mpya zilizojengwa na Serikali ya awamu
ya nane kwa fedha za ahuweni ya uviko 19 Zanzibar, kwa Unguja na Pemba.
IDARA
YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akisoma maelezo ya Jiwe la Msingi la ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu Wilaya ya
Mjini Unguja, baada ya kuifungua rasmin leo 24-4-2023, iliyojengwa kupitia
Fedha za Uviko-19 na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Unguja Mhe.
Idrissa Kitwana Mustafa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said
Dimwa, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar
na Tanganyika
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akikata utepe kulifungua Jengo Jipya la Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu
Wilaya ya Mjini Unguja iliyojengwa kupitia fedha za Uviko-19, ikiwa ni
shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika na
(kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Mohamed
Mussa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Dimwa na (kushoto
kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akimsikiliza Mwanafunzi Hunaina Hamad wa Darasa la Saba wa Skuli ya Msingi ya
Kidongochekundu , alipotembelea Maabara ya Sayansi ya Skuli hiyo baada ya
kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli hiyo uliofanyika leo 24-4-2023, na
(kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela
Mohammed Mussa na (kulia kwa Rais) Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustaf.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akimsikiliza Mwanafunzi wa Darasa la Saba Habal Haji Majid wa Skuli ya Msingi
ya Kidongochekundu , alitowa maelezo jinsi ya kujifunnza kupitia Tehama
alipotembelea chumba cha Komputa cha Skuli hiyo baada ya kuweka Jiwe la Msingi
la Ufunguzi uliofanyika leo 24-4-2023 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiwapongeza Wanafunzi wa Darasa la Saba wa Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu
Wilaya ya Mjini Unguja wakati akitembelea moja la darasa katika Skuli hiyo
baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Skuli hiyo, iliyojengwa kupitia fedha
za Uviko-19 na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.
Idrissa Kitwana Mustafa na (kushoto kwa Rais) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdulgulam Hussein., ikiwa ni shamrashamra za
maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akihutubia wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Msingi ya
Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja, iliyojengwa kwa fedha za Uviko -19,
uzinduzi huo uliofanyika leo 24-4-2023, ikiwa ni shamrashamra Maadhimisho ya
Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika
No comments:
Post a Comment