Habari za Punde

Watakiwa Wazazi Kukuondoa Tofauti Zao za Kitalaka na Badala Yake Washirikiane Kuwalea Watoto Wao Pamoja

Na.Maulid Yussuf. WMJJWW.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imewakutanisha wanandoa walioachana kwa lengo la kuwapa elimu ya namna ya malezi ya pamoja kwa watoto wao.

Amesema ni vyema kuondoa tofauti zao za kitalaka na badala yake washirikiane kuwalea pamoja watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji.

Mkurugenzi Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee bwana Hassan Ibrahim Suleiman ameyasema hayo wakati alipofungua mafunzo ya TULEE PAMOJA kwa Wazazi hao, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano, Sebleni kwa Wazee Mjini Unguja. 

Amesema ni vyema kutambua kuwa kila mmoja baba na mama ana kitu chake katika kumlea mtoto wake, hivyo ni lazima kuangalia na kufikiria suala hilo kwa  faida ya watoto wao.

Amesema watoto mara nyingi wamekuwa ni watu wakuiga mambo mengi  wanapoyaona, hivyo amewataka kuhakikisha wanapokuwa na hitilafu zao, kuhakikisha watoto hawawaoni,  kwani hali hiyo pia inaweza kuwaumiza kisaikolojia.

Amewaomba wazazi na wanandoa nchini, kupunguza hasira kwa kuangalia ndoa zao na watoto wao katika kuwa na malezi bora na huduma, ili kuwanusuru watoto wao kutokana na masuala ya udhalilishaji. 

Naye Mkuu wa Divisheni ya Hifadhi ya  Mtoto katika Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee ndugu Sheikh Ali Sheikh amesema mafunzo hayo yana lengo la kuwashirikisha wanandoa waloachana kujua umuhimu wa kuwalea na kuwahudumia watoto wao.

Amesema kutambua kuwa ubaba na umama  hauwataweza kufutika na wala kuachana kulea pamoja kutokana na kizazi kiliopo kati yao.

Amesema Wizara imegundua kuwa  miongoni mwa changamoto za walioachana ni  kushindwa kutofutisha Ndoa na uzazi, na hivyo kupelekea watoto wao kukosa huduma na  kudhalilika.

Pia amesema wameona kuwa baba na mama wanapoachana vinakuwepo visasi na hivyo kuwapa shida watoto wao kama wao ndio waliopewa talaka.

" hakuna talaka ya mtoto, kuna talaka ya mume kwa mke na sio nyengine, wazazi jitambueni" amesisitiza   Ndugu Sheikh.

Hivyo amesema ni vyema kuangalia na kuona kuwa watoto wanawahitaji wote mama na baba kila mmoja kwa umuhimu wake kwa kuwatunza na kuwahudumia vyema kila kinachitajika kwao.

Wakiwasilisha mada juu ya Familia zilizoachana na mada ya Malezi ya pamoja,  Afisa hifadhi ya  mtoto  bi Khadija Ali Ahmed na Afisa hifadhi ya Watoto ndugu Fatma Maulid Haji  wamesema  masuala ya wazazi wanapoachana mtoto anaathirika kisaikolojia, kuanguka kimasomo, na hata kuwa na uwezekano wa kuwa na tabia mbaya inatokana na kutelekezwa.

Hivyo wamewaomba wanandoa walioachana kujitahidi malezi ya pamoja kuwalea watoto wa kwa mustakbali mzuri wa maisha yao na watoto wao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.