Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud
Othman, ameitika Wizara ya Fedha na Mipango na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar
kufanya juhudi za kuzisambaza vyema tarifa za matokeo ya Sensa sambamba na
kuhamasisha taasisi za Serikali na Binafsi juu ya matumizi sahihi ya takwimu hizo kwa kuwa ni fursa muhimu katika
kuendeleza kukuza shughuli za kibishara na uchumi nchini.
Mhe. Othman ametoa maelekezo hayo hayo huko Ofisini kwake Migombani mjini
Zanzibar alipokabidhiwa nakla za
vitabu kumi na moja vya taarifa tofauti za
matokeo ya Sensa ya mwaka 2022, kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar
Mhe. Saada Mkuya Salim aliyembatana na Kamisaa wa Sensa Zanzibar Balozi
Mohammed Hamza pamoja na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Ndugu Salim Kassim Ali.
Mhe. Othman amesema kwamba iwapo taarifa hizo za matokeo ya
sense zitatumika ipasavyo zitaweza kuleta manufaa makubwa katika nchi hasa katika upangaji wa mipango ya maendeleo
katika shughuli za kibiashara na toaji wa huduma mbali mbali za kijamii katika
ngazi tofauti.
Amesema kwamba jamiii na taasisi za Serikali na binafsi kwa
jumla zinahitaji kuhamasishwa na kuwa na
mwamko juu ya kuwepo haja na umuhimu mkubwa wa kutumia taaisfa hizo katika
masuala mbali mbali na kuwa chachu ya mabadiliko ya kimaendeleo nchini.
Mhe. Makamu amefahamisha kwamba kufanya hivyo pia ni fursa
muhimu kwa serikali katika suala la kuendeleza juhudi za ukusanyaji mapato hasa kwa vile sense hiyo imefanywa kwa utaalamu mkubwa
uliozingatia masuala muhimu yanayohitajhika katika shughuli za kiuchumi na
maendeleo.
Aidha amesema kwamba taasisi zote za serikali ni muhimu
kutumia taarifa hizo katika masuala mbali mbali ya mipango na utoaji huduma
kwenye sekta na maeneo tofauti jambo litakaloongeza ufanisi na kukuza
maendeleo.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salim,
amesema kwamba kunahitajika juhudi kubwa
kubwa ya kutoa elimu na
kuhamasisha taasisi za serikali ili kuwa na mwamko sahihi wa kuzitumia takwimu
zilizopo katika kuandaa mipango yao
mbali mbali.
Aidha Dk. Mkuya amesema pia kuwepo anuani za makazi ( Post
Code) kupitia Sensa hiyo kutasaidia katika juhudi za Serikali za kuendeleza suala
la ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi na usahihi zaidi na kuongeza mapato ya
serikali.
Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa Balozi Mohammed Hamza amsema
kwamba kazi kubwa ya usambazaji wa
matokeo ya taarifa za sense inaendelea na kwamba kupatikana kwa taarifa sahihi
kupitia anuani za makazi kutasaidia pia kuzuia udanganyifu katika suala zima la
ukusanyaji wa mapato.
Wakati huo Mh. Othman amekutana Kamati Mapitio ya sera ya
Maji Zanzibar na kueleza kwamba katika muendelezo bora wa sera ya maji ni vyema
kuwepo mipango sahihi nay a muda mrefu ya maji sambamba na kufahamu kiwango
sahihi cha maji yaliyopo na mahitaji yake kwenye matumizi ili kuwezesha huduma
hiyo kutolewa kwa uhakika .
Aidha ameshauri kwamba ni vyema Mamkala ya Maji kuachiwa kazi
ya kuitunza rasilimali hiyo ili kuifanya kuwa endelevu na kuwepo chombo
kitakachopewa mamlaka na kazi ya kusambaza huduma hiyo kwa watumiaji huku taasisi zenye mwelekeo mmoja na mnaba wa
majukumu kufanya kazi kwa ukaribu zaidi kulimko ilivyo sasa.
Aidha ameshauri kwamba kwa vile kutokana na mamumbile yua
Zanzibar arilimali hiyo kutegemnewa zaidi kutoka ardhini ni vyema kuwepo mpango na mkati madhubuti zaidi utakaosaidia usimamizi bora
wa rasilimali hiyo hasa kwa kuzingatia kwamba kumekuwepo na mabadiliko mkubwa
katika maisha ya watu kuishi kisasa zaidi na mahitaji kuwa makubwa kadri siku
zinavyokwenda mbele.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo chake cha Habari leo tarehe 07.06.2023
Makamu wa kwanza wa Rais Mhe. Othman Masoud Othman akizungunza na Waziri wa Fedha Mhe, Saada Mkuya (Kulia ) alipofika kumkabidhi Nakla za matokeo ya sena kushoto kwa waziri ni Kamisaa wa sensa Balozi Mhammed HamzaImetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo chake cha Habari leo tarehe 07.06.2023
No comments:
Post a Comment