Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amejumuika na Wananchi katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Miembeni

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Jijini Zanzibar alipofika kujumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu  katika Ibada ya swala liyofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) pamoja na Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya Swala ya Ijumaa  iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akiagana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid pamoja na Viongozi wengine mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya  Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Jijini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu wa Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume,mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya  Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Jijini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu] 02/06/2023. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.